Bawa
kubwa la ndege limeokotwa na wananchi jana katika Bahari ya Hindi
kwenye Kisiwa cha Kojani, Pemba. Haijafahamika ni la ndege ya shirika
gani.
Sehemu ambayo inaaminika ni mabaki ya ndege imevuliwa katika bahari ya hindi katika ufukwe wa kisiwa cha kojani pemba.
Bawa
la ndege lililopatikana katika bahari ya kisiwa kidogo cha Kojani huko
kisiwani Pemba, yamezusha mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa kisiwa
hicho huku wengi wakiamini ni bawa la ndege ya Malaysia ambayo ilipotea
bila kujuilikana hatima yake. Ndege ya shirika la Malaysia Airlines
yenye chapa MH370, iliotoweka Machi 8 mwaka 2014 haijawahi onekana hadi
leo.
Ingawa
bado hakuna uhakika ni mabaki ya ndege gani, wataalamu wa usafiri wa
anga wamenza hatua ya awali ya uchunguzi wa mabaki hayo ya ndege.
Taarifa
zinasema tayari maofisa wa usalama wameanza kulifanyia uchunguzi bawa
hilo na huenda si muda mrefu tukapata maelezo ya kutosha kutoka vyombo
vinavyohusika
No comments:
Post a Comment