BARAZA
la Madaktari nchini limetakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na taaluma
ya fani hiyo kwa ajili ya kuleta ufanisi na kutoa huduma kwa wananchi.
Hayo
yalisemwa na Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo wakati akizindua baraza hilo
mjini hapa.
Kombo
alisema taaluma ya udaktari, inaheshimika na ni tegemeo kubwa kwa wananchi
wengi kwa sababu madaktari wanabeba dhima na majukumu makubwa.
Alisema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk Ali Mohamed Shein, imekuwa
ikifuatilia kwa karibu changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo na
kuzipatia ufumbuzi.
‘’Macho ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yapo kwa sekta ya afya ikiwemo madaktari
kuona maslahi yao yanaboreshwa pamoja na nafasi ya mafunzo mara kwa mara,"
alisema.
Alisema
Baraza la Madaktari ni tegemeo la kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za
madaktari pamoja na taaluma hiyo ikiwemo maadili ya kazi.
Alikitaka
chombo hicho, kamwe kisiwavumilie madaktari watakaokiuka maadili ya taaluma
hiyo kwa kuiondolea heshima yake.
Mwenyekiti
wa Baraza la Madaktari, Dk Jamal Adam alisema wamejipanga kuzipatia changamoto
mbalimbali zinazowakabili madaktari pamoja na taaluma hiyo.
No comments:
Post a Comment