Na
Mwandishi Wetu
MASHIRIKA
ya ndege ya nje na ndani yamekubali kushiriki katika maonesho ya ndani ya
utalii ili kutangaza utalii wa Tanzania.
Maonesho
hayo yanayojulikana kwa jina la ‘Swahili International Tourism Expo’ yatafanyika jijini Dar es
Salaam kuanzia Oktoba 13 hadi Oktoba 15, mwaka huu.
Akizungumza
katika hafla ya kutia saini ushirikiano wa kufanikisha maonesho hayo kati ya
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Shirika la Ndege la Ethiopia, Ethiopian
Airlines, Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi amesema maonesho hayo
yanalenga kuitangaza Tanzania kimataifa.
“Mbali ya
Ethiopian Airlines mashirika mengine ya ndege tunayoshirikiana nayo ni Air
Tanzania na Coastal Aviation ambao tufanya nao kazi kwa karibu kuona namna
wageni watakavyofikia maeneo ya karibu na vivutio au maeneo husika,” amesema Mdachi.
Maonesho
hayo yatakayofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere
(JNICC), mbali ya mambo mengine yatasaidia kutoa taarifa za vivutio vya
kiutalii nchini pamoja na mawakala kutoka mataifa mbalimbali kueleza shughuli
zao.
“Kutakuwa
na shughuli mbalimbali ikiwemo ngoma za asili, michezo ya watoto na bidhaa za
kitamaduni. Vilevile zaidi ya washiriki 150 watakuwepo kutoka mataifa zaidi ya
15 ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Mauritius na Shelisheli,” amesema Mdachi.
Kwa
upande wake, Meneja Mkazi wa Ethiopian Airlines, Dahlak Teferi amesema wana
furaha kuwa sehemu ya wadhamini wa maonesho hayo kwa sababu shirika lao
linatazamia kuwa mdau mkubwa wa kutangaza utalii katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki na Pembe ya Afrika.
No comments:
Post a Comment