Watu 24 wameripotiwa kupoteza maisha
nchini Afghanistan baada ya kutokea shambulio la bomu kwenye mji mkuu wa
nchi hiyo wa Kabul.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi wa Afghanistan, Najib Danish amesema licha ya watu 24 kupoteza
maisha kwenye shambulio hilo na wengine 42 wakijeruhiwa.
Polisi nchini humo wamesema tukio hilo lilitokea saa 12:48 asubuhi wakati watu wakielekea kazini na mlipuko ulikuwa mkubwa sana.
Kundi cha Taliban kupitia msemaji wa
kundi hilo, Zabihullah Mujahid limedai kuhusika na shambulio hilo ambalo
Polisi wamesema ni bomu la kujitoa muhanga na walikuwa wamepanga
kulipua mabasi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Usalama wa nchi hiyo.
Baadhi ya majeruhi wa shambulio hilo wakiwa hospitali.
No comments:
Post a Comment