MAKAMU
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema jukumu kubwa la nchi za Afrika ni
kuhakikisha zinaweka mazingira wezeshi ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja
zote.
Samia
ameyasema hayo jana kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Kuwawezesha na Kuwaendeleza
Wanawake Afrika lililoandaliwa na Asasi ya Graca Machel na kufanyika jijini Dar
es Salaam.
Makamu
wa Rais alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuwaendeleza wanawake
bado mazingira hayampi nafasi mwanamke hasa yule anayeishi kijijini.
Aidha,
aliainisha baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na sheria na sera zilizopo
ambazo bado zinawanyima wanawake fursa ya kumiliki ardhi pamoja na haki ya
kurithi hata kama haki hizo zipo kisheria.
“Hii
inatokana na utekelezaji mbaya wa sheria, unaosababishwa na uwepo wa mianya ya ubaguzi kwenye kwenye sheria hizo
jambo ambalo linakinzana na mfumo rasmi wa kisheria zilizowekwa,” alisema.
No comments:
Post a Comment