Unapopita maeneo mengi ya mijini na pembezoni wa miji utakutana na
wafanya biashara wa miwa wanaouza miwa na wanaouza juice ya miwa. Wengi
hununua juisi ya miwa kwa kuwa hufuraia utamu wake. Lakini umeshajiuliza
juisi ya miwa inafaida gani kiafya?
Faida za kiafya za juisi ya miwa
Kunafaida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo;
1. Uwezo wa kuipa miili nguvu kwa haraka "instant kick of energy"
Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na
kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari "sucrose"
ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati
mwingine ukiwa na nguvu au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya
viwandani tafuta juisi ya miwa.
Ingawa jusi ya miwa ina utamu inafaa sana kwa watu wenye kisukari. Hii
ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa
kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa "Low Glycemic
Index". Kutokana na hilo jusi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala
wa vinywaji vingine vya viwandani. Ni mhimu pia kwa watu wenye kisukari
kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa daktari.
3. Juisi ya miwa inasaidia kupunguza matatizo ya kansa
Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium,
potassium, chuma n manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao
husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi
dume "Prostate cancer" na kansa ya maziwa "Breast Canser"
4. Juisi ya miwa huipatia miili protein
Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.
Juisi a miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu
hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono "STDs" na kidney stones.
Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana
Ma-daktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano,
6. Juisi ya miwa husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula.
Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa ch madini ya potassium ambayo husaidia
kuimarisha mmeng'enyo wa chakula. Vilevile juisi ya miwa husaidia
kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo. Vilevile husaidia katika
kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa "constipation".
7.Juisi ya miwa husaidia kuzuia kuoza kwa meno
Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meo kuoza na matatizo
ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hyo kama
unafikiria kwenda kwa daltari kung'arisha meno yako, kunywa juisi ya
miwa mara kwa mara.
8. Juisi ya miwa husaidia kuimarisha ngozi.
Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung'arisha
ngozi. Juisi ya miwa huweza kutumika kama " face mask na scrub" kwa
kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing'arisha na
kuiimarisha.
Hitimisho
Juisi ya miwa inafaida nyingi mwilini, ni muhimu kuhakikisha usafi
katika utengenezaji wake. Juisi ya miwa isiyokuwa salama inaweza ikawa
ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya tumbo na kuhara.
No comments:
Post a Comment