Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, (kulia), akipeana mikono na Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, wakati akipokea msada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya kituo cha Afya Mkoani mjini Kibaha Aprili 29, 2017.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, ameishukuru TANESCO kwa msaada wake wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkoani Mjini Kibaha.
Mhandisi Ndikiro alisema, hatua hiyo yaTANESCO ni ushahidi tosha wa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma afya katika mazingira ya usafi.
"Niseme tu mlichokifanya ni kitu kizuri sana, na ningeshauri taasisi nyingine za umma na binafsi, kutoa sehemu ya faida wanayopata kutokana na shughuli zao na kurudisha kwa umma kwa njia ya kusaidia shughuli za kijamii kama hii ya usafi." Alisema.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi Leila Muhaji alisema, TANESCO kama mtoa huduma ya umeme kwa Wananchi na ikitambua kuwa wananchi ndio wateja wake wakubwa, pia imeona ni busara kusaidia serikali katika kuhakikisha mazingira yanayowazunguka kama vile kituo hiki cha afya yanakuwa safi." Alisema.
Bi. Leila pia alisema, TANESCO imetoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha umma kufanya usafi wa jumla kila mwisho wa wiki. "Tumeungana nanyi leo Jumamosi ambayo ni siku ya usafi, ili tufanye usafi pamoja kwenye kituo chetu hiki cha afya, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, napenda muwashukuru sana na mpokee msada wetu huu mdogo ambao nina hakika utasaidia kwa sehemu fulani katika kuweka mazingira ya hospitali yawe safi." alsiema
Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikiro, aliwaongoza watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Pwani na wachache kutoka makao makuu katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka nyasi kuzunguka mazingira ya kituo hicho cha afya.
Mhandisi Ndikilo, akiwa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akitoa hotuba yake
Bi Leila Muhaji, (katikati), akitoa hotuba yake, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, na Meneja Rasilimali watu TANESCO mkoa wa Pwani, Bi.Nisile Mwakalinga
Wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani
Mhandisi Ndikiro akimshukuru Bi.Nisile, huku Bi. Leila (wapili kushoto) na Bi Salama Juma, ambaye ni Afisa Uhusiano TANESCO
Wafanyakazi hawa wa TANESCO wakiwa wamebeba sehemu ya vifaa hivyo
Mhandisi Ndikiro, (kulia) na Bi. Leila Muhaji wakifyeka majani kwenye eneo la Kituo hicho cha Afya
Wafanyakazi wa TANESCO wakifagia mazingira kuzunguka kituo hicho |
Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akifafanua baadhio ya mambo kwa waandishi wa habari
Watumishi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha, wakifyeka nyasi
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Mhandisi Ndikiro akiwa amenyanyua baadhi ya vifaa alivyokabidhiwa
Watumishi wa kituo hicho cha afya wakikusanya sehemu ya vifaa hivyo
Mtumishi wa kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha, akwia amebeba sehemu ya vifaa hivyo
No comments:
Post a Comment