Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha
Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na
mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko
Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda
cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada
ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha
Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya
mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha
Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akizungumza mara baada ya
kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Picha mbalimbali zikionyesha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha
Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mmiliki wa Kiwanda cha
Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini
Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Desemba 2016, amekutana
na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote
kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.
Katika mazungumzo hayo, Rais
Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania
itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika
kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.
Rais Magufuli amesema kuhusu
kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara
hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka
kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja
kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
Amemtaka Dangote kununua gesi
moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya
kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.
”Iwapo unataka maelezo yoyote
ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala
ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya
ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ” amesema Rais Magufuli.
Dokta Magufuli amesema Dangote
ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake
wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu
ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza
faida kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wake mmiliki wa
Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote
ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa
sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu
ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania
ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.
Katika kuthibitisha hilo, tayari
Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia
saruji yake. Ameongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali
na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania
kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya
nchi ambazo zinapatikana nchini.
Alhaji Dangote amemuhakikishia
Rais magufuli kuwa ataendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania na
kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na
baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine
zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za
uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Katika hatua nyingine Rais Dkt.
John Pombe Magufuli amuapisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher
Olonyokie Ole-Sendeka anayechukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye
amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wengine walioapishwa na Rais
Magufuli ni Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye anakuwa Katibu Mkuu, Wizara
ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo (Kilimo), Dkt. Maria Sasabo Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Dkt. Aloyce K.
Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Bibi
Grace Alfred Martin kuwa Balozi (Mkuu wa Itifaki).
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU.
Dar es Salaam.
10 Desemba, 2016.
No comments:
Post a Comment