Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump |
RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump, ametishia kufutilia mbali sera
ya rais Barrack Obama ya kurejesha uhusiano kati ya Marekani na Cuba
wakati atakapochukua madaraka Januari mwakani.
Trump amesema uamuzi huo utategemea utawala wa kikomyunisti mjini
Havana, kuweka sera ambazo zitaimarisha hali ya maisha kwa raia wa nchi
hiyo, na wale waliochukua uraia wa Marekani na wale wa Marekani.
Utawala wa rais Obama umejitahidi kurejesha uhusiano na utawala wa Havana, baada ya uhasama uliodumu kwa zaidi ya miaka hamsini.
Trump amemtaja marehemu Castro kama kiongozi mkatili wa kiimla ambaye aliwakandamiza raia wake kwa miongo kadhaa.
CHANZO BBC NEWS
No comments:
Post a Comment