NA MWANDISHI WETU, Mara
BARAZA
la Mitihani la Taifa NECTA imeifungia shule ya msingi ya Little Flower
Englishi Medium inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Musoma
kutofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la saba kwa kipindi cha miaka
mitatu mfululizo baada ya kubainika kufanya udanganyifu mkubwa wa majibu
ya matokeo ya darasa la saba katika mtihani ambao umefanyika mwezi
Septemba mwaka huu.
Akitangaza
uamuzi huo wa NECTA katika kikao cha kuchagua wanafunzi wa kujinga na
kidato cha kwanza mwaka kesho, afisa elimu wa mkoa wa Mara Hamis Lisu,
amesema mbali na kituo hicho kufungiwa kufanya mtihani huo katika
kipindi cha mwaka 2017 hadi 2019, pia matokeo yote ya wanafunzi 37
waliofanya mtihani huo mwaka huu katika kituo hicho wilayani Serengeti
pia yamefutwa.
Naye
katibu tawala mkoa wa Mara Bw Adoh Mapunda, akizungumza katika kikao
hicho cha uchaguzi wa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha
kwanza, ameonya tabia ya baadhi ya walimu wakuu wa shule za msingi na
wakuu wa shule za sekondari kujihusisha na vitendo vya udanganyifu, na
kwamba amesema serikali itachukua hatua kali katika kukomesha vitendo
hivyo.
No comments:
Post a Comment