Baadhi ya watu wenye
ulemavu wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao
alipotembelea kituo cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) wakati wa ziara yake Peramiho.
Mhazini
wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA)
Mwl.Elswida Charles
akimkabidhi risala ya kikundi hicho kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt.
Abdallah Possi Peramiho Ruvuma.
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimkabidhi Mwenyekiti wa PEDIPA
Bw.Pius S.Kayombo Kiti Mwendo ili kumsaidia katika shughuli zake za kila siku.
Mwenyekiti wa PEDIPA Bw.Pius S.Kayombo
akiwa katika zoezi la kutumia kiti mwendo alichokabidhiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Dkt. Abdallah Possi alipotembelea kituo hicho Peramiho Ruvuma.
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akikabidhi mashine ya kushonea nguo kwa Mhazini
wa kikundi cha kulelea watu wenye mahitaji maalum cha PEDIPA
Mwl.Elswida Charles
wakati wa ziara yake kituoni hapo Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma.
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa mafuta maalum ya ngozi kwa mmoja wa
washiriki wa wajumbe wa kikundi cha PEDIPA wakati wa ziara yake Ruvuma
Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na Bi.
Cholastika Haule ambaye ni mlemavu wa viungo mara baada ya kumalizika kwa ziara
yake Wilayani Peramiho Mkoa wa Ruvuma. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Na.Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu,
Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii
kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili
kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua kiuchumi.
Dkt.Possi
ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea
Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule
zenye kuhudumia watu wenye
mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye
ulewavu cha Peramiho
Disabled Persons Action (PEDIPA) na
Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika
ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto nyingi za watu wenye
ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua changamoto wanazokabiliana
nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha watu hao katika mipango yote ya
maendeleo.
“Halmashauri
ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu
katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali ya utegemezi na
kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa hawawezi” .Alisema
Mhe.Possi.
Waziri Possi alisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri ziwe na
ubunifu wa miradi ya maendeleo itakayo walenga watu wenye ulemavu, “Ni vyema
sasa kuwe na jitihada za makusudi za kuunda miradi maalum kwa ajili ya kuwapa
nafasi za ushiriki ili kujitafutia vipato na kuyakabili mazingira yao,
ikumbukwe wakina mama waliachwa nyuma kwa muda mrefu ila baada ya kupaza sauti
zao tunaona sasa wanasikika hivyo hivyo iwe kwa watu wenye ulemavu” Alisitiza
Dkt.Possi.
Aidha
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Dkt.Osca Albano alisisitiza kuyapokea
maelekezo yote ya Naibu Waziri Mhe.Possi kwa vitendo na kumhakikishia kuwa
Wilaya yao itakuwa mstari wa mbele katika kulitekeleza hilo.
“Sisi
tunafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Halmashauri hivyo ni vyema tukalichukua
hilo kuangalia namna tunavyoweza kuliweka katika mipango yetu yote ya maendeleo
ili kuwasaidia na kufikia lengo la serikali,” alisema Dkt. Albano.
Nae Katibu
Tawala Wilaya ya Songea Bw. Edmund Siame aliomba halmashauri zote ziwe zinatoa
mrejesho mapema juu ya maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu huku Mwalimu
Elswida Charles anayehudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum akimweleza Dkt.
Possi kuwa watu wenye ulemavu wanafarijika kutokana na jitihada anazofanya
kuwainua watu wenye ulemavu.
No comments:
Post a Comment