JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”
Ofisi ya Inspekta
Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:
DAR ES SALAAM.
30 /11/2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
SINGIDA AFARIKI DUNIA.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016
katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda,
mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi
cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato
cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro
mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake
alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa
Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003),
Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (2016).
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa
Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa
ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa
Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa
pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.Amen.
Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment