MSAMA AMUOMBA RADHI RADHI MWAKYEMBE - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, June 24, 2016

MSAMA AMUOMBA RADHI RADHI MWAKYEMBE

 Mmiliki  wa Gazeti la Dira ya Mtanzania Alex Msama akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati akimuomba radhi Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrson Mwakyembe kutokana na habari iliyochapishwa kwenye gazeti lake la toleo namba 423 na 424.
Alex Msama akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MMILIKI wa Gazeti la Dira ya Mtanzania Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrson Mwakyembe kutokana na habari iliyochapishwa kwenye lake  toleo namba 423 na 424.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akiomba radhi kwa Waziri Mwakyembe, Msama alisema habari hizo zilikosa weledi na umakini kutoka kwa mhariri na mwandishi.

Alifafanua kuwa toleo namba 424 lilikuwa na habari yenye kichwa kisemacho "Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani wakati toleo namba 423 ilikuwa na habari inayosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2.

"Habari hizo zimenisikitisha mimi binafsi na kamba Dk. Mwakyembe ni kaka yangu wa karibu na nimefahamiana naye kwa muda mrefu. Hivyo naomba aniwie radhi kutokana na usumbufu alioupata pamoja na familia yake,"alisema Msama.

Aliongeza tayari kama kampuni imechukua hatua za kumsimamisha kazi mhariri na mwandishi wa habari hiyo wakati uchunguzi ukifanyika kabla ya kuchukua hatua zaidi za kinidhamu.

Msama alisema kilichomsikitisha zaidi hata yeye mwenyewe ni taarifa hizo kumhusisha moja kwa moja Dk. Mwakyembe badala ya kampuni yake ya Power Pool.

Alisema kama ambavyo amekuwa akimheshimu Dk. Mwakyembe ataendelea kumheshimuna kutambua mchango wake mkubwa kwa taifa hili huku akisisitiza kuomba radhi kwa kilichotokea.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here