Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu
akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa UDART, David Mgwasa mara
alipowasili Makao Makuu ya UDART Jangwani Dar es Salaam leo asubuhi
kukabidhi msaada huo.
Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu akielekea eneo la tukio la kukabidhi msaada huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula
kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza
dua hiyo Mussa Salum
Mwenyekiti wa Makampuni ya Simon Group
Robert Kisena aliyetoa msaada huo akizungumza wakati akimkaribisha
Makamu wa Rais kuzungumza na wananchi. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania, Shamim Khan, Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum Mussa
na Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam, William
Masanja.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum Mussa (kushoto), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Chakula kilicho kabidhiwa.
Waumini wa dini ya kiislamu wakisubiri kukabidhiwa msaada huo uliotolewa na UDART.
Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu
(kushoto), akimkabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa
Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo Tanzania
(Chawaumavita), James Mnyankole. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya
Simon Group, Robert Kisena.
Hapa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Dar es Salaam, Bakwata, Pilli Mwale akipokea msaada huo.
Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu
(kushoto), akimkabidhi boksi lenye tambi, Mwakilishi wa Kituo cha
kusaidia waathiriwa wa dawa za kulevya cha Sober House Kigamboni, Pilli
Missanah
Makabidhiano yakiendelea.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Dar es Salaam, Bakwata, Pilli Mwale akitoa neno la shukurani
Dua la kufunga hafla hiyo likifanyika.
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan
amewataka wazazi na walezi wa watoto wenye mtindio wa ubongo kuwalea
watoto hao bila kuchoka kwani ndio taifa letu.
Mwito huo ameutoa jijini Dar es Salaam
leo asubuhi wakati akikabidhi msaada wa chakula uliotolewa na Udart kwa
ajili ya ya makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji wakiwemo yatima na
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
"Msichoke kuwalea watoto hawa ambao ni
bahati kutoka kwa mwenyezi mungu kwani msingekuwa nao pengine
msingekuwepo hapa leo" alisema Suluhu.
Suluhu aliishukuru kampuni ya Udart kwa
msaada huo kwa waislamu kwa ajili ya futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhan
na akatumia fursa hiyo kuwaomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza
kutoa msaada wa namna hiyo hasa katika kipindi hiki cha mfungo.
Chakula alicho kikabidhi ni sukari, unga wa ngano, sembe, mchele, tambi, tende, mafuta ya kula na majani ya chai.
Katika hatua nyingine makamu wa Rais
aliwataka viongozi wa makundi hayo zaidi 18 yaliyopata msaada huo
kuhakikisha msaada huo unawafikia waliokusudiwa na si vingenevyo.
Makamu wa Rais pamoja na kukabidhi
msaada huo pia alikagua mabasi ya mwendo wa haraka yanayomilikiwa na
Udart ambapo alisema yatasaidia kuwapunguzia wananchi adha ya usafiri
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon
Group aliyetoa msaada huo alisema baada ya kupokea barua ya maombi ya
kusaidia makundi hayo aliguswa na kuamua kusaidia chakula hicho na vitu
vingine vikiwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni 60.
Alitaja baadhi ya vituo vilivyopata
msaada huo kuwa ni New Hope Group, Khiyari Ophans Centre Chang'ombe,
Al-Madina Tandale, Hisani Mbagala Maji Matitu, Safina- Mbagala Nzasa,
Mwandariwa-Boko, Mwana cha Vingunguti, New Life- Kigogo na Mwana Mbagala
kwa Mangaya.
Alivitaja vituo vingine kuwa ni New
Life-Kigamboni, Sunat- Yombo Vituka, Chama cha Wazazi wa watoto wenye
ulemavu wa ubongo (Shivawata), Tasodedi-Viziwi wasio ona, TLB-Walemavu
wa macho, Albino-Watu, Soba House, Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Dar es
Salaam, Jumuiya ya Vijana wa Kiislam Dar es Salaam na Kampala
Internation University-Muslim Student Association
No comments:
Post a Comment