Kamishna wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathaniel Methew
akiwaeleza waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu
kuboreshwa kwa mifumo ya utoaji huduma kwa wananchi kwa kuongeza
matumizi ya TEHAMA hali iliyochangia kuongeza tija kupitia kituo cha huduma kwa mteja kilichopo Makao Makuu ya Wizara hiyo na Katika Ofisi zote za Kanda.kushoto ni Msajili wa Hati Msaidizi
Msajili
wa Hati Msaidizi toka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw.
Apollo Laizer akitoa wito kwa wananchi kuzingatia sheria na kanuni
wanapotaka kumiliki Ardhi ili kuepusha migogoro ya Ardhi. Kulia ni
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Bw. Nathaniel Methew.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi uliolenga kutoa ufafanuzi kuhusu maboresho katika kuwahudumia wananchi kupitia kituo cha huduma kwa mteja.
Frank Mvungi-Maelezo.
WIZARA
ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi imehudumia wananchi 41,932
kati ya Novemba, 2015 hadi sasa kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kamishina wa Ardhi Msaidizi Nathanael Methew wakati wa mkutano na vyombo vya habari, uliofanyika
kwenye ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO), ambapo alisema lengo la
kituo hicho ni kuongeza tija na kasi ya kuwahudumia wananchi.
“Tunahudumia
watu zaidi ya 400 kwa siku na kwa mwezi ni wateja 8,386 tangu
tuanzishe kituo cha Huduma kwa Mteja hapa Wizarani,” alisema.
Akifafanua
Methew amesema kuwa kituo hicho kimeweza kusaidia kuondoa malalamiko
mengi ya wananchi dhidi ya Wizara katika kushughulikia kero na
changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika sekta ya Ardhi.
Akitaja
faida za kituo hicho Methew amesema kuwa kimeongeza imani kwa wananchi
na kuondoa uwezekano wa huduma kutolewa kwa upendeleo.
Kituo hicho pia kimepunguza kwa kiasi kikubwa muda ambao wateja wanasubiri kupata huduma.
Katika
hatua nyingine Methew amesema kuwa Wizara inao mpango wa kufungua vituo
vya huduma kwa wateja kwenye ofisi zote za Ardhi za Kanda.
Naye
Msajili wa hati msaidizi Apollo Laizer alitoa wito kwa wananchi
kuzingatia sheria na kanuni wanapotaka kumiliki ardhi ili kuepuka
migogoro inayohusu sekta hiyo.
Aliongeza
kwamba kituo hicho, kinatoa huduma za utawala wa ardhi,upimaji na
Ramani,Mipango Miji na Vijiji,Maendeleo ya Nyumba,Huduma za Usajili wa
Hati, nyaraka mbalimbali na malalamiko ya wateja.
No comments:
Post a Comment