HIKI NDICHO ALICHOKISEMA PROF. MAJI MAREFU KUHUSU KUKWEPA KODI - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, December 10, 2015

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA PROF. MAJI MAREFU KUHUSU KUKWEPA KODI

1 

MBUNGE wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM), amekanusha maneno yaliyotolewa na baadhi ya watu kuwa anahusika na ukwepaji wa kodi na hivyo kuisababishia hasara Serikali kama ilivyojitokeza kwa baadhi ya wafanyabiashara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ngonyani ambaye ni maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, alisema hajawahi kukwepa kodi na wala hatarajii kufanya hivyo kwa kuwa anajua umuhimu wake na kuongeza kuwa wanaomtuhumu kufanya hivyo wanataka kumchonganisha na Serikali katika kipindi hiki ambacho Rais Dk. John Magufuli anahimiza wananchi kulipa kodi.


Profesa Maji Marefu alitoa kauli hiyo baada ya chombo kimoja cha habari kuripoti, kwamba anamiliki gari la kifahari lenye thamani ya Sh milioni 300 ambalo hakulilipia kodi.


“Kuna gazeti moja limeandika nimekwepa kodi ya gari langu la kifahari ninalolimiliki kwa sasa. Nimesikitishwa na habari hiyo kwa sababu gari hilo nililinunua kwa shilingi milioni 173.612, nikalilipia kodi ya shilingi milioni 69.3, nikalilipia bima ya shilingi milioni 8.5 na kisha nikalilipia namba maalumu za jina langu la Maji Marefu kwa gharama ya shilingi milioni tano.


“Kabla ya kulipia namba maalumu, awali gari hilo aina ya Land Cruiser Super Challenger lilikuwa na namba T 666 DFS ambazo nilikuwa nimezilipia bila kukwepa kodi.


“Sasa inapotokea mtu anasema namiliki gari ambalo nimekwepa kulilipia kodi, naumia kwa sababu naonewa bila sababu za msingi.


“Kwahiyo, nitalifikisha suala hili mahakamani ili wanaosema nilikwepa kodi, waje na ushahidi wao na mimi nitapeleka ushahidi wangu wa nyaraka zote nilizonazo.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here