Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani usiku wa kuamkia leo katuka Uwanja wa Lugogo Cricket Oval, Kampala, Uganda.
Diamond akiimba kwa hisia.
Madansa wa Diamond wakiendelea na makamuzi.
...Akiwauliza jambo mashabiki wake wa Uganda (hawapo pichani).
...Akicheza sambamba na madansa wake.
...Akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Diamond akiwa amesimama na madansa wake baada ya shoo.
USIKU
wa kuamkia leo katika Uwanja wa Cricket wa Lugogo, Uganda, staa wa
muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' alifunika kwa
kupiga shoo kubwa na ya kihistoria.
Diamond aliyekuwa ameongoza na madensa wake, muda mwingi aliwakosha
mashabiki hao kwa kuwapigia nyimbo zake zote kali zinazotamba kama vile
Kesho, Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyingine kibao.
Baada ya kufunika shoo hiyo.
Diamond
atarejea jijini na moja kwa moja kujiandaa na shoo nyingine kubwa na ya
kihistoria itakayofanyika Sikukuu ya Krismasi (Desemba 25, mwaka huu)
ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem
jijini Dar.
Kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live, Diamond atapiga live kwa kutumia
vyombo nyimbo zake zote kali ikiwa ni pamoja na hii ya Utanipenda ambayo
ni habari ya mjini kwa sasa.
Mbali na Diamond katika shoo hiyo pia atakuwepo mkali wa nyimbo za
Singeli, Msagasumu ambaye tagonga nyimbo zake zote kali zinazobamba kama
vile Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Naipenda Simba na nyingine nyingi.
Baada
ya Msagasumu, Mashabiki pia wataburudika na shoo kutoka kwa wakali wa
kucheza nyimbo Afrika Mashariki, Wakali Dancers ambapo watakinukisha
mwanzo mwisho kwa kutoa burudani ya kucheza ngoma zote zinazobamba ndani
na nje ya nchi kwa staili za kipekee.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
No comments:
Post a Comment