Na Mwandishi Wetu, Katuma Blog tz
RAIS
John Magufuli amefuta rasmi sherehe za miaka 54 ya Uhuru zinazotarajiwa
kufanyika Desemba 9, mwaka huu, na badala yake kuagiza siku hiyo iadhimishwe kwa mtindo wa kufanya usafi ili kudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu.
Agizo
hilo, lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi
Ombeni Sefue, wakati akizungumza na uongozi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili
(MHN) na waandishi wa habari.
Alisema
ugonjwa wa Kipindupindu chanzo chake kikubwa ni uchafu, hali inayoonyesha
kuwa bado Tanzania kuna haja kubwa ya kushughulikia uchafu ili kuondokana na
magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
“Kwa
mujibu wa Rais Magufuli, siku ya Desemba 9, ambayo kila mwaka Tanzania
husherehekea kama Siku iliyopata Uhuru wake, badala ya kushuhudia shamrashamra
za magwaride, halaiki na ndege za kivita kama ilivyozoeleka, badala yake
wananchi wote watasafisha mazingira,” alisisitiza Sefue.
Aliwataka
Wakuu wa Mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na makatibu tawala
wote nchini, kuanza kujiandaa na kuweka mikakati ya namna ya kufanya usafi huo
katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuandaa vifaa vya kusafishia mazingira.
Alisema
gharama zitakazotumika kwa ajili ya maandalizi ya sherehe hizo, rais Magufuli,
atazipeleka katika maeneo mengine yatakakuwa na mahitaji.
Alisema
kwa mujibu wa Dk Magufuli, hataki kusikia baada ya Desemba kuna mgonjwa wa
kipundipundu sehemu na kwamba endapo kutakuwa na mgonjwa anayesumbuliwa na
ugonjwa huo, mkoa husika uongozi wake watawajibika na kujieleza.
No comments:
Post a Comment