ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amefungua ukurasa mpya kwa kuwa
kiongozi wa kwanza wa kisiasa kumtembelea Ikulu Rais Dkt John Pombe Magufuli na kufanya naye mazungumzo ikiwa ni wiki chache tangu
kiongozi huyo alipoapishwa kuongoza nchi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoufikia
mtandao huu, katika mazungumzo hayo, Prof. Lipumba ametumia nafasi
hiyo kwa kumpongeza Rais Magufuli kufuatia ushindi wake wa kishindo
alioupta katika uchaguzi mkuu uliopita.
Mbali na hilo Prof. Lipumba pia
ameipongeza hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge
la 11 mjini Dodoma 30, 2015 kutokana na kugusa maeneo mbalimbali
yanaaakisi moja kwa moja maisha ya watanzania sambamba na kusimamia
uwajibikaji wa viongozi wote.
No comments:
Post a Comment