Sehemu
ambako utaanzia upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar
es salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za
barabara za lami kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli
la kutumia fedha shilingi bilioni nne zilizopaswa kutumika kugharamia
Shamrashamra za siku ya Uhuru Desemba 9, 2015 kutumika kufanya upanuzi
wa barabara hiyo.PICHA NA IKULU.
.....................................................................................................
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa
kutumika kugharamia shamra shamra za siku ya Uhuru ambazo zingefanyika tarehe
09 Desemba 2015, kutumika kufanya upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco
jijini Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za
barabara za lami.
Tayari fedha
hizo kiasi cha shilingi bilioni nne zimepelekwa kwa wakala wa barabara hapa
nchini TANROADS kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara
moja
Akizungumza na
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi PATRICK MFUGALE Ikulu Jijini Dar es Salaam,
Dkt. Magufuli ametaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na
adha ya msongamano wa magari katika
barabara hiyo
Kujengwa kwa
njia hizo kutaifanya barabara ya Morroco hadi Mwenge kuwa na njia tano.
Wakati huo huo,
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mstaafu wa
Chama Cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba Ikulu Jijini Dar es salaam.
Katika
Mazungumzo hayo Prof. Lipumba amempongeza Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kwa kutoa
hotuba nzuri ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliyokonga nyoyo za Watanzania.
Kwa Upande wake
Rais Magufuli amempongeza Prof. Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga
ufisadi na amemtakia heri katika shughuli zake.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es Salaam.
30
Novemba,2015
No comments:
Post a Comment