Na Jacquiline Mrisho- maelezo
Idadi ya wagonjwa wa
kipindupindu jijini Dar es salaam imepungua kufikia wagonjwa kumi na mbili (12)
kwa mkoa mzima, huku wilaya ya Temeke ikiwa na wagonjwa saba,Kinondoni wagonjwa
wanne na Ilala ikiwa na mgonjwa mmoja
.
Haya yamezungumzwa na
Mratibu wa Magonjwa ya kuambukiza wa
Jiji la Dar es salaam Bw. Alex Mkamba
ofisini kwake leo akielezea jinsi gani mkoa umefanikisha kupambana na
kipindupindu kwa kuzingatia usafi katika jiji.
Ameongeza kuwa katika
kufanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu wametoa mafunzo juu ya mbinu shirikishi ya namna ya kujikinga
na kipindupindu kwa watendaji wa mitaa na pia imewahimiza kukagua maeneo yao na
kuwapa kibali cha kufunga maeneo ya biashara au maeneo yatoayo huduma za
chakula yasiyozingatia usafi.
Akielezea kuhusu
huduma kwa wagonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam mratibu huyo amesema jiji lina
dawa za kutosha za kuhudumia wagojwa ipasavyo
kwa kuwapatia huduma bora zaidi kuendana na kasi ya maambukizi yaliyopo.
“ hata leo Shirika la
Afya Duniani (WHO) limetoa dawa za kusafishia maji (Water Guard) maboksi 45 kwa
kila wilaya” Mkamba alifafanua.
Aidha alisema
serikali imejipanga katika kudhibiti maambukizi mapya kwa kuwapima wagonjwa
kabla na baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini
na aliwashauri wananchi kubadili tabia kwa kuhakikisha usafi unafanyika
pia kuchemsha maji na kuufanya usafi kuwa
ni tabia yao ya kila siku.
Mpaka sasa jumla ya watu
55 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment