TUME
ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imemtangaza Dk John Pombe
Magufuli Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mshindi wa kiti
cha Urais kwa kupata kura 8,082,935 sawa na 58.46% na kumshinda Mpinzani
wake ndugu Edward Ngoyai Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) aliyepata kura 6,072,848 sawa na 39.97%.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji (Mstaafu) Damian Lubuva aliwatangaza wagombea wengine na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Anna Elisha Mghwira (ACT Wazalendo) kura 98,763 sawa na 0.65%, Chief Lutalosa Yemba (ADC) kura 66,049 sawa na 0.43%, Hashim Rungwe Spunda (Chaumma) kura 49,256 sawa na 0.32%.
Wengine ni Kasambala Janken Malik (NRA) kura 8,028 sawa na 0.05%, Lymo Macmillan Elifatio (TLP)8,158 sawa na 0.05%, Dovutwa Fahim Nasoro (UPDP) kura 7,785 sawa na 0.05%.
Wapiga kura walioandikishwa walikuwa 23,161,440. Waliojitokeza kupiga kura ni 15,589,636 sawa na 67.31%. Kura halali zilizopigwa ni 15,193,862 sawa na 97.46% na Kura zilizokataliwa ni 402,248 sawa na 2.58%..
No comments:
Post a Comment