Mkurugenzi
Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa taasisi ya Young Scientists Tanzania
(YST), Dk. Gosbert Kamugisha, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) leo hii wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya siku tatu ya miradi
na ubunifu wa kisayansi uliofanywa na wanafunzi kutoka shule 120
nchini. Maonyesho hayo yatafikia kilele Ijumaa Agosti 7, 2015. (Picha
zote na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com).
Mwanzilishi Mwenza wa YST, Joseph Clowry, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo hii.
Makamu
wa Rais wa kampuni ya kuchakata mafuta na gesi ya BG Tanzania, John
Ulanga, akizungumzia udhamini wao katika maonyesho hayo ya YST. Kampuni
hiyo imetoa kiasi cha Dola 200,000 kudhamini maonyesho ya mwaka huu.
Naibu
Balozi wa Ireland nchini, Brian Noran, akizungumzia maendeleo ya tafiti
za kisayansi kwa taifa lolote duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
na Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini.
Mwalimu
Geofrey Ndunguru (kulia) na mwanafunzi Yussuph Mwenda kutoka Shule ya
Sekonari ya Wavulana Songea nao wanashiriki maonyesho hayo kuzungumzia
Uchambuzi wa Mtazamo wa Wanafunzi Wasioona kuhusiana na Sayansi.
Mwanafunzi
Gladness Mpelemba (kulia) wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari
Sumaye mjini Morogoro akielezea kuhusu utafiti wao wa ‘Kutumia Njia za
Asili za Kupanga Uzazi Kupunguza Madhara kwa Wanawake’. Kushoto ni
mwenzake Glory Crispine.
Mojawapo ya utafiti uliofanywa na wanafunzi Saada Abeid na Zaina Maliki wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mtwara.
Majaji
wakiwa kazini leo hii ili kuwapata washindi watakaotunukiwa zawadi
mbalimbali hapo kesho ambapo Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Alhaj Ali
Hassan Mwinyi, ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
………………………………………………..
RAIS mtaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi leo
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya kazi za kiugunduzi
na kisayansi zilizofanywa na wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
Katika uzinduzi huyo, zaidi ya wanafunzi 240 na walimu 120
kutoka bara na visiwani kwa siku tatu wataonesha kazi zao za ugunduzi na
utafiti wa kisayansi kama vile kemia, fizikia na hesabu, biologia na teknologia
pamoja na teknologia ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wanasayansi Chipukizi
Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha alisema kazi hizo zitajumuisha maeneo
mapana ya kisayansi pamoja na kutafuta ufumbuzi kwa masuala kama afya, Kilimo
na usalama wa chakula.
Dk. Kamugisha alitaja maeneo mengine kama vile mawasiliano
na uchukuzi, nishati na mazingira, elimu, mahusiano na matatizo ya kijamii.
“ Kama njia ya kuwapa moyo vijana wetu wabunifu, zawadi
zitatolewa kwa wanafunzi wenye kazi nzuri za kisayansi na teknologia,” alisema
Dk Kamugisha.
Naye Makamu Rais wa Kampuni ya uchimbaji wa mafuta na gesi
(BG), John Ulanga ambao ndiyo wadhamini wa maonesho hayo alisema zaidi ya
wanafunzi 60 watazawadiwa fedha.
Alisema wanafuzi sita watakaoshinda alama za juu
watazawadiwa udhamini wa kusoma vyuo vikuu kusomea shahada za sayansi na
teknologia na kuendelea kufanya kazi za kisayansi katika maisha yao.
Alisema washindi wa jumla wa maenosho hayo mbali na kupewa
pesa na udhamini wa masomo ya vyuo vikuu, pia watashinda zawadi ya kwenda
nchini Ireland mwakan kuiwakilisha Tanzaniaa katika mashindano ya kimataifa.
“ YST 2015 ni onesho la wanafunzi wenye vipaji katika
sayansi, pia ni ushahidi unaoonyesha kuimalika kwa ujuzi wa walimu ambao ni
walezi wa wanafunzi hao,” alisema Ulanga.
Aliongeza kuwa maonesho hayo yataanza kesho (leo) na
kumaliza kesho kutwa na yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee na watu
wote wanakaribishwa.










No comments:
Post a Comment