NDESAMBURO AKUTANA NA DK. SLAA JIJINI DAR ES SALAAM - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, August 5, 2015

NDESAMBURO AKUTANA NA DK. SLAA JIJINI DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA Mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo, maarufu kama "Ndesa Pesa", amekutana jijini Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye ilielezwa hapo awali na chama chake kuwa kwa sasa yuko mapumzikoni, Dkt. Willibrod Slaa, nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Ndesamburo alifuatana na makada wenzake wa chama hicho, baadhi yao ni Meya wa Manispaa ya Moshi ambaye pia ni mgombea ubunge (mtarajiwa), wa jimbo hilo, Japhary Michael.
Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa ya nini wamezungumza, ingawa makada hao wa CHADEMA walikuwa jijini kuhudhuria mkutano mkuu maalum wa chama hicho uliomteua Waziri Mkuu wa zamani Mh. Edward Lowassa, kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya mwavuli wa muungano wa vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA. Mgombea mwenza aliyeteuliwa ni Mh. Juma Duni Haji.  
Kwa hisani ya JIACHIE BLOG

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here