Martin
Evavest na Vernance Robinsoni wakinyanyua tuzo yao juu ya Automatic House Contro System
kwenye Maonesho ya wanasayansi chipikizi kutoka shule za sekondari ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Diamond Jubileeleo jiji Dar es Salaam
Washindi
wa mwaka jana Dhariha Amour Ali na Salima Khalfan Omar kushoto katika ni
Hatim Karimjee wakionyesha vyeti vyao walivyotunikiwa katika Maonesho hayo.
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akifungua Maonyesho ya 5 ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati akifungua Maonyesho ya 5 ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha
akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Balozi wa Kenya nchini
Tanzania Chirau Ali Mwakwere kabla ya kufungua maonyesho hayo mwishoni
mwa wiki.
Baadhi ya wadau wa sayansi walioudhuria katika mashindanio hayo.
RAIS
mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, amewataka walimu katika
shule za msingi na sekondari kutumia lugha ya Kiswahili kufundisha sayansi,
kwani lugha hiyo inaeleweka vizuri.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Tano ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule
za sekondari nchini jijini Dar es Salaam jana, Alhaj Mwinyi amesema Kiswahilini
lugha inayoeleweka vizuri, si kwa wanafunzi tu,bali hata kwa watu wengine,
hivyo ni vyema walimu wakaweka mkazo katika kuitumia kwenye masomo ya sayansi.
“Lakini
nataka niwaambie, walionieleza kwa Kiswahili, pamoja na utafiti wao kuwa katika
lugha ya Kiingereza, walifafanua vizuri sana na nikasema ‘aah, kumbe Kiswahili
kinaweza kutumika kufundisha vizuri sayansi,” alisema.
Aliongeza kusema
kwamba, yeye wakati anaingia darasa la tano, mwalimu wake wa sayansi alikuwa
rais wa Scotland, lakini alimfundisha sayansi kwa Kiswahilina ndio msingi wake mkubwa
wa kulifahamu vyema somo la sayansi.
Akizungumzia
maonyesho hayo yaliyoandaliwa na kuratibiwa na taasisi ya Young Scientists
Tanzania (YST), Alhaj Mwinyi amesema ni jitihada nzuri za kuandaa wataalam wa
kesho katika sayansi.
Maonyesho hayo
yalifanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee yakishirikisha jumla ya wanafunzi
240na walimu 120 kutoka shule 120 nchini.
“Hii inafurahisha
kuona watoto wadogo wanaichambua sayansi kwa kufanya tafiti hizi nzuri kabisa
na kwa hakika nawapongeza sana waandaaji na muendelee hivyo hivyo kuandaa
kizazi cha sayansi,” alisema Alhaj Mwinyi.
Wadhamini wakuu
wa maonyesho hayo, Kampuni ya BG Tanzania, wamesema wataendelea kudhamini
maonyesho yajayo ili kuweka hazina ya wataalamu wa sayansi wa kesho.
“Sisi
tunajihusisha na utafiti wa gesi na mafuta, tunahitaji wanasayansi wataalamu ambao
lazima tuanze kuwekeza sasa, ndiyo maana katika maonyesho ya mwaka huu tumetoa
Dola 200,000 na mwakani tutatoa kiasi kingine ambacho kinaweza kuwa kama hicho
au zaidi,” alisema Makamu Rais wa BG Tanzania, John Ulanga, ambaye anayeshughulikia
Sera na Masuala ya Uhusiano.
Naye
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan, ambao ni wadhamini wa
maonyesho hayo, alisema nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada za YST kama ambavyo
wamekuwa wakifanya tangu maonyesho hayo yalipoanza mwaka 2011.
Katika maonyesho
hayo ya tano, wanafunzi wa Mzumbe Sekondari kutoka Morogoro, Edwin Luguku na
John Method, ndio walioibuka washindi wa jumla kutokana na utafiti wao usemao “Kupunguza
Matumizi ya Mifuko ya Plastiki Tanzania” (Reducing The Use of Plastic Bags in
Tanzania).
Kwa ushindi
huo, vijana hao ambao mbali ya kupata medali na tuzo na wamepata zawadi ya
hundi ya Shs. 1 milioni. Walikabidhiwa zawadi zao na Rais mstaafu Alhaj Ali
Hassan Mwinyi.
Washindi wa
pili walikuwa Emmanuel Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na
utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling Ecto-parasites’, ambao wamepata
medali na tuzo pamoja na hundi ya Shs. 1 milioni, ambapo walikabidhiwa zawadi
zao na Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan.
Zawadi nyingine
kwa washiriki wa maonyesho hayo zilikuwa katika makundi manne ambayo ni Sayansi
ya Baolojia na Ikolojia (Biological and Ecological Sciences) iliyodhaminiwa na
Taasisi ya Afya Ifaraka; Sayansi ya Kemikali, Hisabati na Fizikia (Chemical,
Mathematical and Physical Sciences) iliyodhaminiwa na Taasisi ya Fizikia
(Institute of Physics);
Sayansi ya Kijamii na Kitabia (Social and Behavioural
Sciences) iliyodhaminiwa na shirika la Concern; na Teknolojia (Technology)
iliyodhaminiwa na Karimjee Jivanjee Foundation.
Katika makundi
hayo, mbali ya kupatiwa medali na tuzo, washindi wa kwanza walipata Shs.
500,000, washindi wa pili Shs. 300,000 na washindi wa tatu Shs. 200,000.
Aidha,
wadhamini wengine wa maonyesho hayo walitoa zawadi mbalimbali ambao ni Songas,
Read International, Solaris, Spicenet, Karimjee Jivanjee, Masumin Printways, First Car Rental, Vernier, na Human
Development Innovation Fund (HDIF).
Washindi wa tuzo maalum:
Tuzo ya Kupenda Sayansi ya Songas: Venance Msechu na Martin
Oisso kutoka St. Jude Sekondari, Arusha na utafiti wao ‘Automatic House Control
System’.
Tuzo ya Read International: Evance Marumbwe na Sara
Ismail kutoka Mtapika Sekondari, Mtwara na andiko lao la ‘Mbinu za Ufundishaji
Zinachochea Kukua kwa Taaluma (Do Teaching Methods Influence Academic Performance?)
Tuzo ya Solaris: Emmanuel Lemalali na Emmanuel
Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method For Controlling
Ecto-parasites’.
Tuzo ya Masumin Printways: Maregesi Nyamajeje na Peter
Kailembo kutoka Mwasele Sekondari, Shinyanga na andiko lao la ‘Designing a
Temperature Sensor’.
Tuzo ya First Car Rental: Augustino Simon na Felister
Stanley kutoka Butimba Day, Mwanza na utafiti wao wa Who Votes In Mwanza? (Nani
Anayepiga Kura Mwanza?).
Tuzo ya Vernier: Tunu Ngajilo na Ally
Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
Tuzo ya HDIF: Tunu Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya
Sekondari na utafiti wao wa Automatic Irrigation System.
Tuzo ya Spicenet: Geofrey Ndunguru na
Yusuph Mwenda, Songea Boys, na utafiti wao wa Analysis of Blind Students
Attitude Towards Science (Uchambuzi wa Hulka ya Wanafunzi Wasioona Katika Mwelekeo
wa Sayansi).
Washindi wa makundi mbalimbali:
Sayansi ya Baolojia na Ikolojia:
1. Mariam
Ngaula na Latifa Mussa kutoka Kilakala Sekondari, Morogoro na utafiti wao wa ‘The
Scarcity of Water in Morogoro’.
2. Saada
Abeid na Zaina Maliki wa Mtwara Girls na utafiti wao wa ‘Leaching effects for
Maize growing In Mtwara’.
3. Latifa
Hamad Ali na Salma Hussein Haji kutoka Kiembe Samaki Sekondari, Zanzibar na
utafiti wao wa ‘Exploring Lippia Asperifolia Leaves (Mpambaake) On Anaemic
Pregnant Women’.
Sayansi ya Kemikali, Hisabati na Fizikia:
1. Adil
Abdallah na Kevin James kutoka Loyola Sekondari, Dar es Salaam na utafiti wao
wa ‘Micro Plastics In Drinking Water’.
2. Maryam
Salim na Betty Pentzel kutoka Popatlal Sekondari, Tanga na utafiti wao wa ‘The
Effects Of Chemical Hair Products And Its Solution’.
3. Patrick
Boniface na Jacob John kutoka Mara Sekondari na utafiti wao wa ‘First Principle
Of Integration’.
Sayansi ya Kijamii na Kitabia:
1. Latifa
Mohamed na Raphael F. Nyamhanga wa Mtwara Technical na utafiti wao wa ‘Is ICT
the solution to poor academic performance?’
2. Nancy
George na Christermine Christopher kutoka Debrabant Sekondari, Dar es Salaam na
utafiti wao wa How To Reduce Road Accidents In Kilwa Road (Jinsi ya Kupunguza
Ajali za Barabarani Katika Barabara ya Kilwa).
3. Aloyce
Botto na Devis Mafuru wa Tumbi Sekondari, Kibahana utafiti wao wa ‘Swahili
Language As A Medium For Learning And Instructions In Tanzania’.
Teknolojia:
1. Venance
Msechu na Martin Oisso kutoka St. Jude Sekondari, Arusha na utafiti wao ‘Automatic
House Control System’.
2. Tunu
Ngajilo na Ally Salum kutoka Mbeya Sekondari na utafiti wao wa Automatic
Irrigation System.
3. Salivius
Simon na Derick Deusdedit kutoka St. Joseph Kolping Sekondari na utafiti wao wa
‘Carrying Capacity Governing Device’.
Tuzo ya Karimjee Jivanjee:
Washindi ambao
watafadhiliwa masomo ya shahada ya kwanza chuo kikuu ni Petro Samson Ndegeleki na
Juma Joshua Wiliam kutoka Nassa Sekondari ambao utafiti wao ulihusu ‘How
Different Natural Fertilizers Affect the Growth Of Maize’. Washindi hao pia watagharamiwa
safari ya kwenda Dublin, Ireland kuhudhuria maonyesho ya sayansi ya BT YSTE
Januari 2016.
Washindi wa Pili wa jumla:
Emmanuel
Lemalali na Emmanuel Sanga kutoka Tanga Technical na utafiti wao wa ‘A Simple Method
For Controlling Ecto-parasites’.
Washindi wa Jumla 2015:
Edwin
Luguku na John Method wa Mzumbe Sekondari na andiko lao la ‘Reducing the use of
plastic bags in Tanzania’.
Hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa Shule za Sekondari nchini kutoka bara na visiwani waoneshana ‘ubavu’ wa kuwasilisha kazi zao za ugunduzi na utafiti wa kisayansi walizozifanya.
Tafiti hizo za kisayansi ni pamoja kemia, fizikia na hesabu, biologia na teknologia pamoja na teknologia ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wanasayansi Chipukizi Tanzania (YST) Dk. John Ulanga alisema kazi hizo zilijumuisha maeneo mapana ya kisayansi pamoja na kutafuta ufumbuzi kwa masuala kama afya, Kilimo na usalama wa chakula.
Dk. Kamugisha alitaja maeneo mengine kama vile mawasiliano na uchukuzi, nishati na mazingira, elimu, mahusiano na matatizo ya kijamii.
“ Kama njia ya kuwapa moyo vijana wetu wabunifu, zawadi zitatolewa kwa wanafunzi wenye kazi nzuri za kisayansi na teknologia,” alisema Dk Kamugisha.
Naye Makamu Rais wa Kampuni ya uchimbaji wa mafuta na gesi (BG), John Ulanga ambao ndiyo wadhamini wa maonesho hayo alisema zaidi ya wanafunzi 60 watazawadiwa fedha pindi maonesho hayo yatakapomalizika.
Alisema wanafuzi sita watakaoshinda alama za juu watazawadiwa udhamini wa kusoma vyuo vikuu kusomea shahada za sayansi na teknologia na kuendelea kufanya kazi za kisayansi katika maisha yao.
Alisema washindi wa jumla wa maenosho hayo mbali na kupewa pesa na udhamini wa masomo ya vyuo vikuu, pia watashinda zawadi ya kwenda nchini Ireland mwakan kuiwakilisha Tanzaniaa katika mashindano ya kimataifa.
“ YST 2015 ni onesho la wanafunzi wenye vipaji katika sayansi, pia ni ushahidi unaoonyesha kuimalika kwa ujuzi wa walimu ambao ni walezi wa wanafunzi hao,” alisema Ulanga.
Aliongeza kuwa maonesho hayo yataanza kesho (leo) na kumaliza kesho kutwa na yatafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubelee na watu wote wanakaribishwa.
No comments:
Post a Comment