CHAMA cha
madereva wa mabasi na malori nchini, kimesema kitaendelea na mkakati wake wa
mgomo nchi nzima, iwapo serikali haitatatua suala la kupatiwa mikataba mipya ya
kazi.
Chama
hicho kimesema kitakutana na wanachama wote nchini, kesho (Jumapili), ili kutoa
tamko la kuitisha mgomo.
Mkutano
uliofanyika Juni 21, mwaka huu na uliwakutanisha chama hicho, Wizara ya Kazi na
Ajira, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na
kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu, na kutoa maamuzi ya wamiliki kuanza kuwapa
mikataba madereva.
Katibu wa chama hicho, Rashid Saleh anasema katika mkutano huo kikao kilipitisha makubaliano ya kuanza kutumika kwa
mikataba hiyo, ifikapo Julai mosi, mwaka huu.
Katibu wa
Umoja wa Wamiliki wa Mabasi nchini (Taboa), Enea Mrutu, jana alisema kuwa mgomo
huo ulipaswa kufikishwa katika kamati iliyoundwa na waziri mkuu, kabla ya
kuchukua maamuzi ya kutangaza kugoma.
No comments:
Post a Comment