1. Mkurugenzi wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo, Thomas Samkyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki
ya wakulima Tanzania
(TADB), uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu JK Nyerere.
1.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akikata utepe kuzindua benki ya Maendeleo ya Kilimo.
2.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya Maendeleo ya Kilimo.
1. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akifuatilia uzinduzi wa
benki ya Maendeleo ya Kilimo, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo
Bi Rosebud Kurwijila, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa benki, bwana Thomas
Samkyi, na kutoka kushoto ni Waziri wa Kilimo, Stephen Wasira akifuatiwa na
Waziri wa Fedha, Bi Saada Mkuya.
1. Mwenyekiti wa Bodi
ya benki ya Maendeleo ya Kilimo, Bi Rosebud Kurwijila, akizungumza wakati wa
uzinduzi wa benki.
1. Wageni waalikwa
wakifuatilia uzinduzi wa benki ya Maendeleo ya Kilimo
Rais
Kikwete azindua benki ya kwanza ya Wakulima Tanzania
Dar
es Salaam, 6/8/2015: Rais Jakaya Kikwete leo amezindua benki ya kwanza ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania, ambayo inalenga kuanzisha mtizamo mpya wa
kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau mbali mbali, kuangalia kila
mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake, pamoja na kuwa na ubunifu katika
kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda mrefu, ya kati na muda mfupi kwenye
sekta ya kilimo. Benki hiyo
inatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa sekta ya kilimo ambayo imeajiri
zaidi ya aslimia 70 ya Watanzania.
Akizungumza
katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais Kikwete amesema changamoto
zinazowakabili wakulima nchini ndizo zilizosababisha serikali yake kuanzisha
benki hii ili kuwakomboa wakulima kwenye umaskini ili waweze kuzalisha
kibiashara na sio kwa kwa kujikimu.
‘Awali huduma
za kifedha na mikopo kwa wakulima hazikuwepo kabisa na hivyo kupelekea tija
kwenye kilimo kuwa chini, uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo nao ukawa
chini ya viwango vya Afrika na hata dunia, hivyo ya uzinduzi wa benki hii
unafungua ukurasa mpya wa mapinduzi ya kilimo nchini’ alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete
pia aliwaasa wakulima kutumia vyema fursa ya uanzishwaji wa benki hii akisema
kwa sasa kilimo kinachangia asilimia 25 ya pato la taifa, huku asilimia 35 ya
bidhaa tunazouza nje ni za kilimo.
‘Serikali
imetoa mtaji wa kuanzisha benki wa jumla ya shilingi bilioni 60, na tunatarajia
kuingia hati fungani ili kuiongezea benki mtaji kwa jumla ya shilingi bilioni
800’ anasisitiza Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mkuu wa benki, Bwana Thomas
Samkyi, alisema dhumuni kuu la uanzishaji wa benki hiyo ni kuboresha tija
katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo kwa kuunganisha nguvu za wadau
mbalimbali ili kuwezesha uendelezaji wa miundombinu ya kilimo kama miradi ya
umwagiliaji, usafirishaji, uhifadhi, mindombinu ya masoko, n.k. ambayo
inachangia maendeleo ya sekta ya kilimo.
‘Uanzishwaji
wa benki hii unalenga kuziba mianya mikubwa ya ukopeshaji kwenye kilimo ambayo
inaachwa na benki za biashara, ili kuchochea kukua kwa sekta ya kilimo, kwa
kutoa mikopo na huduma nyingizezo za uwezeshaji wa kilimo kwa wakulima, ambao
wengi wao hawana uwezo wa kupata huduma za kibenki’ alisema Bw. Samkyi.
Akieleza zaidi kuhusu uanzishwaji wa benki hiyo,
Bwana Samkyi alisema Benki ya Wakulima itakuwa msitari wa mbele katika kusukuma
shughuli za kilimo pamoja na kuchagiza benki na taasisi nyingine za kifedha
kushiriki katika kuwezesha shughuli za kilimo.
‘Benki
hii imeundwa ili kutoa mikopo kwa masharti nafuu, pamoja na kutoa huduma
nyinginezo zitakazoongeza uwezo wa wakulima kukopa na kuzalisha. Ili
kufanikisha haya, benki inabidi iwe na vyanzo endelevu vya fedha za kutosha
kwani nchi hii ni kubwa na wadau wa benki ni wengi sana. Lengo kuu ni kubadili kilimo cha Tanzania kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha kibiashara’ alisema Bw. Samkyi.
Benki hii pia
inatarajiwa kuwa ni kiungo muhimu cha utekelezaji wa mageuzi ya awamu ya pili
ya sekta ya kifedha, na vile vile kuboresha maendeleo ya kilimo nchini
ikizingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 pamoja na mipango mbalimbali ya
maendeleo ya miaka mitano mitano, Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Kilimo, na
Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA), pamoja na sera mbali
mbali za Serikali zinazohusu sekta ya kilimo.
Kuhusu
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
Benki ya Maendeleo ya kilimo Tanzania (katika kuanzishwa kwake) ni taasisi
mpya ya kifedha iliyoanzishwa na serikali kwa madhuni ya kuboresha huduma za
kifedha ikiwa ni pamoja na huduma nyinginezo katika sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Benki hii imeanzishwa ili kufikia malengo ya taifa
yaliyoafikiwa katika Tanzania Vision 2025, kusudio likiwa ni kuwezesha na
kutosheleza upatikanaji wa chakula, kuchochea kilimo cha biashara, pamoja na
kuleta maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umasikini.
No comments:
Post a Comment