UWOYA AWATAKA WANAWAKE KUTORUDISHWA NYUMA NA MFUMO DUME - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, August 4, 2015

UWOYA AWATAKA WANAWAKE KUTORUDISHWA NYUMA NA MFUMO DUME

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYnvs6nDAJDFLdiQlCWmTMln6cE6HyPBZwHQaoIYfRyXZqBMZgRgOoRCm_dL9aBAAmdRymDaKiQ5n6yesLVIbohviuq7hBMZ7bWilJP3R-yhjuzqW-DRW8kv8MjbLer4OMT8CLKmev0Deg/s1600/DSC_0046.JPG
MSANII wa filamu Irene Uwoya ambaye ameshinda nafasi ya kuwania ubunge wa viti maalum vijana mkoani Tabora kupitia CCM  amewataka wanawake wanaowania nafasi ya Ubunge na Udiwani kupitia vyama mbalimbali vya siasa kutorudishwa nyuma na mfumo dume.
 
Msanii huyo alitangazwa kuibuka na ushindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.
 
Kwa sasa anaingia katika nafasi ya kutafuta idhaa ya vijana wa CCM Taifa ili kujihakikishia nafasi katika bunge lijalo na hivyo amevuka hatua ya kwanza muhimu.
 
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi juzi, Uwoya alisema wanawake wanaowania nafasi ya Ubunge katika majimbo na wale wanaowania nafasi ya Udiwani katika kata wanakumbwa na changamoto mbalimbali kubwa ikiwa ni uwezo wa kupambana na mifumo dume.
 

Katika mchuano huo aliyemfuata alikuwa ni Mariam Shamte aliyepata kura 3 huku Zahara Muhidin Michuzi akipata kura 2.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here