MBUNGE wa Viti Maalumu Chadema, Chiku Abwao ndiye atakayepeperusha
bendera ya ACT kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa mjini katika uchaguzi mkuu
ujao, huku akitamba atambwaga mbunge anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter
Msigwa (Chadema).
Mbali na Abwao aliyejiunga na ACT Wazalendo hivi karibuni, Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chadema, Abuu Changawa (Majeki) naye amekiacha
Chadema na kujiunga ACT Wazalendo.
Akizungumza jana, Abwao aliyewahi kuwa mbunge wa NCCR-Mageuzi, alisema;
“nimeondoka Chadema baada ya kubanwa kila kona na Mchungaji Msigwa akidhani
kwamba mimi nilikuwa Chadema kwa sababu ya kutaka cheo.”
Akizungumzia sababu zilizomtoa Chadema na kumpeleka ACT Wazalendo, Majeki alisema; “katika uchaguzi mkuu wa 2010 yapo mengi yaliahidiwa na mbunge anayemaliza muda wake Mchungaji Msigwa lakini hayakutekelezwa.”

No comments:
Post a Comment