Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Unguja ndugu Mbarouk Mrakib katikati
akizungumza na Waandishi wa habari huko ofisini kwake Bububu kuhusu
mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuomba kupatikana kwa Kamanda Mpya
wa UVCC Taifa baada ya Mzee Kingunge kuvuliwa Ukamanda huo. Kulia kwake
ni Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini Canal Msaafu Masoud Ali Khamis
na kushoto ni Mjumbe wa Kamati tendaji UVCCM Wilaya Khadija Ramadhan
Abdu. Picha na Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar.
Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Unguja ndugu Mbarouk Mrakib akizungumza na
Waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Bububu kulia Mjumbe
wa Kamati tendaji UVCCM Wilaya Khadija Ramadhan Abdu.
Baadhi
ya wanachama wa UVCCM wakimpongeza Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya
Mfenesini-Unguja ndugu Mbarouk Mrakib (hayupo pichani) mara baada ya
kuzungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake Bububu.
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 21/08/2015
Baraza
kuu Taifa la Umoja wa Vijana CCM limeombwa kumtamfuta Mtu wa kuchukua
Nafasi iliyoachwa wazi ya Ukamanda Mkuu wa UVCCM Taifa ili kuongeza kasi
ya kuutafuta ushindi wa CCM katika uchaguzi unaokuja.
Kupatikana
kwa Kamanda huyo Mkuu kutachochea zaidi Kasi na ari ya mchakato wa
Kampeni kuelekea ushindi wa CCM katika uchaguzi huo.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini-Zanzibar ndugu
Mbarouk Mrakib alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari huko
ofisini kwake Mfenesini.
Amesema
UVCCM Wilaya inapongeza kwa kuvuliwa wadhifa wa Ukamanda Mkuu Taifa
Mzee Kingunge Ngumbale Mwilu kutokana na Kauli zake zinazokinzana na
Chama na hivyo kushauri hatua za haraka zichukuliwe kupatikana Mrithi
wake.
Aidha
ameongeza kuwa hatua iliyochukuliwa na CCM ya kumuenguwa Edward Lowasa
katika nafasi ya Urais kupitia CCM inafaa kupongezwa kutokana na kasoro
alizokuwa nazo mgombea huyo.
“Sisi
wenyewe Tulimuunga Mkono Lowasa kipindi kile lakini baada ya kuelezwa
Mapungufu yake na Viongozi wetu tumegundua hafai kabisa na Chaguo sahihi
ni Magufuli pekee”Alifahamisha Mrakib.
Amefahamisha
kuwa Siasa za Tanzania zinahitaji Viongozi Wasafi, Waadilifu na
Wasiopenda Dhulma wala Ufisadi na kwamba kiongozi aliyepitishwa na CCM
Dkt, John Pombe Magufuli ndio chaguo sahihi.
Aidha
amedai kuwa Chama cha Mapinduzi tayari kimeshajipatia ushindi kutokana
na kutekeleza vyema Ilani yake na kwamba Wanachama na Wananchi kwa
ujumla watakipigia kura za ndio bila hata chembe ya Shaka.
Hata
hivyo Mrakib ambaye aligombea nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la
Mtoni na kushindwa alisema Mipango yake kwa sasa nikuhakikisha anatoa
kila aina ya Ushirikiano ili Wagombea wote kutoka Chama hicho washinde
katika Uchaguzi unaokuja.
Mrakib
aliwapongoza Vijana waliojitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali
kupitia chama hicho ambapo anaamini walioshinda wataweza kukipeperusha
Vyema chama hicho ili kupata ushindi wa kishindo.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment