"PRESS RELEASE" TAREHE
10.08.2015
MTU MMOJA MKAZI WA NSANSA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DAVID MWAKIPESILE (60) ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA
KICHWANI NA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
09.08.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSANSA, KATA YA
NGONGA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA MHANGA ALIVAMIWA NA
WATU HAO WAKATI ANARUDI NYUMBANI AKITOKEA KWENYE MATEMBEZI KISHA KUMJERUHI.
MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA WILAYA YA
KYELA KWA MATIBABU.
CHANZO CHA MAUAJI HAYO INASADIKIWA
KUWA NI IMANI ZA KISHIRIKINA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. UPELELEZI UNAENDELEA PAMOJA NA MSAKO WA
KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA, JINSI
YA KIUME, MIAKA KATI YA 20-27, ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUKAMATWA AKIWA AMEIBA PILIPIKI
MC 811 AFJ AINA YA T-BETTER MALI YA THOBIUS ALLANUS YENYE THAMANI YA TSHS
1,800,000/=.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
09.08.2015 MAJIRA YA SAA 19:45 USIKU HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO,
TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA
KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA
MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO LA KWANZA KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI WAKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA MICHAEL KIBONA (55) MKAZI WA MLOWO ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE
09.08.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA MLOWO, KATA YA
MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA
GARI MARA BAADA YA AJALI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. UPELELEZI UNAENDELEA
IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
TAARIFA ZA MISAKO:
WATU WATATU WAKAZI WA KIJIJI CHA
MASIANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHAMLA MAHUNDOLA (20) 2. YUNGE LUHUNZA
(25) NA WANGU D/O MKUWA (21) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 09.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO
MKALI ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA MASIANO, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA,
MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZI
Imesainiwa na:
[AHMED Z.MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment