Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre)
Brigedia Jenerali Anselim akiongea na waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu miradi mbalimbali iliyotekelezwa na shirika hilo
inayodhamiria kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo utengenezaji wa
matrekta madogo( power Tiller) ambayo yanalenga kumkomboa mkulima hapa
nchini kwa kuondokana na matumizi ya jembe la makono.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre) Brigedia Jenerali
Anselim.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe akiongea na Waandishi wa
Habari (hawapo pichani) umuhimu wa kutoa habari za kuelimisha kwa jamii
hasa zitakazowawezesha kuwajengea uwezo wa kimaarifa na kuwainua kichumi
kupitia elimu hiyo.
Mhandisi Mkuu Msanifu Albert Wikedzi akiwaonesha waandishi wa Habari (Hawapo pichani) aina mbalimbali za sanifu zinazofanyika katika shirika hilo, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika kiwanda hicho Mjini kibaha.
.Mhandisi
Mkuu wa Karakana kutoka Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative
Technology Centre) Ayoub Mnzava akiwaonesha waandishi wa habari trekta
ndogo (Power Tiller) iliyotengenezwa kwa lengo la kuongeza uwezo wa
wazalishaji wa mazao ya kilimo kote nchini.
Mkuu
wa Kitengo cha Usubiaji Mhandisi Anderson Ole Zakaria akiwaeleza
waandishi wa habari namna kitengo hicho kinavyofanya kazi ili kukidhi
mahitaji ya kiwanda ambapo alisema kitengo hicho kinayeyusha hadi tani
2.5 za chuma zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotoka
katika shirika hilo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre)
Brigedia Jenerali Anselim akiwaonesha waandishi wa habari moja aina ya
gari la kivita lililotengezezwa na shirika hilo.
.Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la NYUMBU (Tanzania Automative Technology Centre)
Brigedia Jenerali Anselim (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
waandishi wa habari waliokuwa katika ziara hiyo,kulia ni Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga
Taifa Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe na kushoto ni mwandishi mwandamizi
wa Channel Ten, Kibwana Dachi.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
No comments:
Post a Comment