Aliyekuwa
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa shinyanga ndugu HAMIS MNGEJA
pamoja na kada maarifu wa chama hicho bwana JOHN GUNINITA wametangaza Rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na chama cha
democrasia na meendeleo CHADEMA ambacho kipo ndani ya ukawa. Katika
mkutano unaoendelea baina ya makada hao wa CCM na wanahabari Jijini Dar
es salaam wamesema kuwa wamechoka kuona chama kinatumia ubabe na mabavu
kuwasimika watu ambao hawana uwezo wa kuiongoza hii nchi na kuacha
viongozi wenye uwezo jambo ambalo wamesema hawawezi kulivumilia milele.
Akizungumza
mwenyekiti huyo wa shinyanga MNGEJA amesema kuwa chama cha mapinduzi
sasa huu ndio mwisho wake baada ya kukataa kufanya mabadiliko ndani ya
chama chao jambo ambalo limewafanya watanzania kukichoka na kuitaji
mabadiliko nje ya chama hicho.
'Mngeja ambaye alikuwa mfuasi wa
Edward lowasa amesema kuwa hali iliyotokea dodoma katika mkutano wa
kufanya uteuzi hali ya Mwenyekiti kuingia na majina yake matano mfukoni
na kukataa ushauri wa viongozi na wanachama ni jambo ambalo lilionyesha
udhaifu mkubwa ndani ya chama hicho hasa pale walipoamua kutumia silaha
na vyombo vya usalama kuwatawanya wanachama waliokuwa wanaihitaji haki
itendeke.
Akiangumzia mgombea wa chama cha mapinduzi JOHN
MAGUFULI mngeja amesema kuwa Kiongozi huyu ni sawa na LEARNER
anayejifunza kuongoza nchi kwani hajawahi hata kuwa balozi wa nyumba
kumi kupitia chama hicho ,hivyo watanzania hawako tayari kuwajaribu watu
katika nafasi kubwa kama ya Urais.Mngeja
anasema kuwa kama viongozi wa CCM wanahitaji kukijenga chama lazima
watengue maamuzi hayo na kuwaomba radhi wanachama wa chama hicho na
kisha kuchagua mtu ambaye anaweza kukivusha chama hicho tofauti na hapo
chama hicho kinakwenda kufa.Mngeja anasema kuwa kama wana ccm watahitaji mambo mengine waite mdahalo na viongozi hao wakaseme yale yote yaliyotokea dodoma STORY KAMILI ITAKUJIA |
No comments:
Post a Comment