ALIYE VAMIA STAKISHARI NA KUUA POLISI AJISALIMISHA - KATUMA BLOG tz.

HABARI ZA HIVI PUNDE

KWA HABARI ZA UHAKIKA NA KUAMINIKA


Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, August 13, 2015

ALIYE VAMIA STAKISHARI NA KUUA POLISI AJISALIMISHA

Wakati jeshi la polisi nchini Tanzania kwa kushirikiana na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam wakiendelea na msako mkali kuwasaka wale wote waliohusika na mauaji ya askari katika kituo cha polisi cha STAKISHARI,Hatimaye mtuhumiwa mmoja ambaye alikuwa anatafutwa na polisi kwa kuhusiaka na tukio hilo amejisalimisha makao makuu ya jeshi la polisi akiambatana na familia yake.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kamishna wa polisi wa kanda hiyo SULEMAN KOVA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni ZAHAQ RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA,ambapo amesema kuwa mtuhumia huyo alijisalimisha makao makuu ya jeshi la polisi akiwa na wake zake wawili baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa anatafutwa kwa hali na mali na jeshi la polisi.

Katika Taarifa ya polisi wakati wakielezea mafanikio ya polisi kuhusu tukio hilo iliyotoka terehe 20 mwezi wa saba ilimtaja ndugu ZAHAQ RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA kama mmoja wa vinara wa tukio lile .
Mtuhumiwa huyo anayedaiwa kuwa msaidizi mkuu namba mbili wa kiongozi wa kundi hilo lililovamia kituo cha polisi stakishari tarehe 12 mwezi wa saba anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi.

Aidha katika msako wa polisi wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wengine wawili waliohusika na tukio lile ambao wametajwa kwa majina kama—
1-RAMADHAN HAMIS miaka 18 mkazi wa Mandimkongo
2-OMARY OMARY AMIRI miaka 24 mkazi wa mbagala.

Jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here