Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia mradi wake wa kuwajengea Uwezo Wabunge na Watumishi
(LSP) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP kwa
mara ya Pili mwaka huu limeratibu Bunge la Vijana kwa kushirikisha
Wanafunzi zaidi ya 100 kutoka Taasisi za Elimu ya Juu hapa Nchi ambao ni
viongozi katika Serikali zao. Bunge hilo ambalo limeanza Jumamosi
tarehe 15 Julai, 2015 na linatarajiwa kumalizika tarehe 19 Julai 2015
Mbunge wa Bunge la Vijana
Shughaib Abdi (CBE) akielezea baadhi ya mapungufu yaliyopo katika
Muswada huo wakati wa Mjadala wa kujadili Muswada huo Bungeni
Wajumbe wa Bunge la Vijana wakishiriki Vikao vya Bunge hilo Mjini Dodoma
Waziri Mkuu katika Bunge la
Vijana kwa mwaka 2015 Alexandra Wasonga (ARDHI) akijibu Maswali ya papo
kwa papo Bunge wakati wa Kipindi cha Masuali kwa Waziri Mkuu
Waziri kivuli wa Vijana kutoka
Kambi Pinzani kwenye Bunge la Vijana Bi. Joyce Shirima akielezea baadhi
ya Mapendekezo ambayo yanastahili kuingizwa kwenye Muswada wakati wa
Majadiliano Bungeni
Daudi Maneno (MUST) nae akitoa dukuduku lake wakati wa Majadiliano Bungeni
Mwanasheria Mkuu katika Bunge la
Vijana kwa mwaka 2015 Gama Zulu Leonidas (SAUT) akiwasilisha Muswada wa
Serikali wa Kuanzisha sheria ya Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2015
Bungeni jana.
Spika wa Bunge la Vijana kwa mwaka 2015 Baraka Thomas (UDSM) akiongoza vikao vya Bunge
Bakari Ibrahim (MKWAWA) akiwasilisha Mchango wake kuhusu Muswada huo Bungeni
No comments:
Post a Comment