
UJUMBE maalum wa
vijana 37 kutoka Taasisi ya Nelson Mandela Foundation ya Afrika ya Kusini,
umeanza safari ya kuukwea Mlima Kilimanjaro.
Lengo la kupanda
mlima huo ni kuhamasisha wadau mbalimbali nchini mwao na Pembe ya Afrika
kujitokeza kuchangia fedha kuzisaidia familia maskini nchini.
Mkurugenzi wa
taasisi hiyo, Sello Hatang, aliiambia NIPASHE jana katika mahojiano maalum
kwamba njia pekee ya wao kumuenzi Rais kwanza Mwafrika mweusi kuiongoza Afrika
ya Kusini; Nelson Mandela, ni kuzinusuru kaya maskini barani Afrika kwa
kuziwezesha kunufaika na sehemu ya michango yake ambayo hutolewa kama fungu
maalum la misaada ya kibinadamu.
Alisema mpango
wao wa kuichagua Tanzania kunufaika na misaada ya taasisi hiyo kwa kupanda
Mlima Kilimanjaro, ni kuzihamasisha taasisi nyingine za utoaji wa misaada ya
kibinadamu pamoja na wadau mbalimbali duniani kuona umuhimu wa kutumia vizuri
rasilimali walizonazo kusaidia jamii inayowazunguka badala ya kutegemea
wahisani kutoka nchini za Magaharibi.
Mhifadhi Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), Erastus Lufungulo, alisema kuwa
idadi ya watalii kutoka mataifa mbalimbali wanaotaka kupanda Mlima
Kiliamanjaro, imekuwa ikiongezeka kila mwaka.
Awali,
Mkurungenzi wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Allen Kijazi, aliishukuru
Taasisi ya Nelso Mandela, kwa kutambua
mchango wa Tanzania kwa nchi ya Afrika ya Kusini wakati wa kupigania uhuru wa
taifa hilo na kuamua kurejesha fadhila kwa kuutumia mlima Kilimanjaro,
kuchangisha fedha za kuzisaidia kaya masikini lakini pia kuvitangaza vivutio vya
utalii vyaTanzania duniani kote.
Kwa mujibu wa
Kijazi, ujio wa vijana hao wa Afrika ya Kusini utasaidia kuongeza pato la taifa
lakini pia utaingazaTanzania kimataifa kupitia sekta ya utalii.
No comments:
Post a Comment