JESHI la Polisi, Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, limeongeza vikosi vingine vya jeshi hilo ili kuongeza nguvu
katika mapambano dhidi ya matukio ya uhalifu likiwamo la ujambazi katika kituo
cha polisi Stakishari.
Katika tukio hilo lililotokea Julai 12 mwaka huu kituoni hapo, watu saba wakiwamo askari wanne wa na raia watatu, walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakiwamo watoto.
Katika tukio hilo lililotokea Julai 12 mwaka huu kituoni hapo, watu saba wakiwamo askari wanne wa na raia watatu, walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa wakiwamo watoto.
Askari akiimarisha ulinzi katika kituo cha polisi cha Stakishari kilichovamiwa na majambazi juzi.
Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman
Kova, anasema kuwa operesheni kali ya kuwasaka watuhumiwa wa tukio hilo
inaendelea.
Kova anasema wanashirikiana na mikoa mingine ya jirani ikiwamo ya Pwani na Tanga ili kufanikisha msako huo.
Anasema, jeshi hilo limeendelea kupokea taarifa nyingi kutoka kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuonyesha ushirikiano wao dhidi ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment