VIJANA 3,000 nchini wanatarajia kupatiwa mafunzo ya namna ya kubadili mitazamo yao
hasi na kuwa chanya hivyo kuwa kichocheo cha maendeleo katika jamii
inayowazunguka.
Mafunzo hayo
yatafanyika kwa siku nne mfululizo kuanzia Julai 26 hadi 29, mwaka huu katika
ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano na shirika la
kimataifa la IYF tawi la Tanzania.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa IYF, nchini, Jeon Hee Yong, alitaja
baadhi ya masomo ambayo yatafundishwa katika kambi hiyo ya kubadilisha fikra
mpya, kuwa ni uwezo wa kujitambua, tamaa na kujitawala, hekima, mabadiliko na kushirikiana, moyo na furaha.
"Kambi hiyo
ya mafunzo ni kwa ajili ya Watanzania wote kuanzia wenye umri wa miaka 16 na
kuendelea wakiwamo walimu huku washiriki watakabidhiwa vyeti vitakavyowasaidia
katika masuala ya ajira.
Aliongeza kuwa
pia washiriki watapata fursa ya kujifunza lugha mbalimbali za kigeni kikiwamo
Kiingereza na Kichina na hivyo kuwasaidia katika kupata ajira.
No comments:
Post a Comment