Ni mamilioni ya Watanzania sasa hivi wako kwenye subira ya kujua ni mgombea gani wa Urais atakaeuwakilisha UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ambao ni muunganiko wa vyama mbalimbali vya upinzani Tanzania.
Hapa millardayo.com leo namnukuu Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria pia wa CHADEMA aliyeongea haya maneno Geita kanda ya ziwa >>>
‘Tumeshapata mgombea Urais wa UKAWA, ameshapatikana na mnamfahamu vizuri sana na mnampenda sana na ni mtu anaejulikana dunia nzima kwa msimamo wake, hatujamtaja jina najua na nyie mnataka nimtaje….. simtaji ila mnamfahamu vizuri sana’
‘Sababu gani simtaji ni kwa sababu tunatafuta mgombea mwenza wake, tukimtaja sasa hivi mtatuuliza na mwenza? tutawaambia ngoja tukamtafute? tunatafuta mgombea mwenza anaeheshimika nchi hii na ni lazima atoke Zanzibar katiba yetu ndivyo inavyosema, tukimpata tutaitisha mkutano na Television zote Tanzania siku nzima itakua ni siku ya Dr. Slaa !!
ahhh nimetoa siri?!!!! hapana hapana hapana….‘ – Tundu Lissu.
No comments:
Post a Comment