Rais wa Marekani Barack Obama
akiwa na bibi yake Mama Sarah Obama kushoto na dada yake Auma Obama
katika chakula cha jioni na wanandugu wa familia ya Obama nchini Kenya
Baba mzazi wa Barack Obama ni mzaliwa wa Kenya.
Rais Barack Obama wa Marekani
akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi kwa ajili ya kufungua
mkutano wa Kimataifa wa kibiashara, Ugaidi na haki za
binadamu unaofanyika nchini humo kabla ya kuendelea na ziara yake
nchini Ethiopia.(PICHA KWA HISANI YA MASHIRIKA YA KIMATAIFA)
Rais Barack Obama wa Marekani
akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi
Rais Barack Obama wa Marekani akisalimiana na dada yake Auma Obama mara baada ya kushuka kwenye Ndege.
Rais Barack Obama wa Marekani
akisalimiana na mwenyeji wake Rais wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta mara
baada ya kushuka kwenye ndege wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Rais Barack Obama wa Marekani
akifurahia jambo na mwenyeji wake Rais wa Kenya Mh. Uhuru Kenyatta mara
baada ya kusaini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Rais Barack Obama wa Marekani
akipunga mkono huku akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Kenya Mh.
Uhuru Kenyatta mara baada ya kusaini kitabu cha wageni alipowasili
kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Airforce 1 Ndege ya Rais Obama
ikiwa kwenye uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi mara baada
ya kumshusha Rais Barack Obama wa Marekani.
No comments:
Post a Comment