King Nahh akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,jana
MTOTO mwenye kipawa cha ajabu katika
kutoa ushauri wa kujijengea uwezo wa kujiamini anayezidi kujipatia
umaarufu mkubwa duniani, Lonnie Hudson maarufu kama ‘King
Nahh’(Pichani), ametua jijini Dar es Salaam , jana.
King Nahh aliambatana na baba yake mzazi ,
Nyeeam Hudson ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa taasisi isiyo ya
kiserikali ya Wisdom Partners.
Kesho mtoto huyo atafanya kongamano
kubwa la watoto na wazazi katika Ukumbi wa Urafiki leo ambapo nia na
madhumuni ni kuamsha hisia za watu ambao wamekata tamaa katika masuala
mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.
Akikabidhiwa shada la mauwa uwanjani hapo
King Nahh akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya kuwasili uwanjani hapo
Meneja wa King Nahh akisisitiza jambo kwa wanahabari
King Nahh akicheza ngoma ya utamaduni
King Nahh akizungumza na wananchi katika viunga vya uwanja wa ndege
Akiwa amepozi na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo
Akisaini kitabu cha wageni katika Supermarket ya Uchumi
Akimlisha keki mmoja kati ya wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
Akilishwa keki na msanii nyota wa filamu, Iluminata Alfonce ‘Dotnata’
Akikabidhiwa
‘token’ na Meneja wa Uchumi Supermarket kwa ajili ya kununulia bidhaa
katika kipindi atakachokuwa nchi, pembeni yake ni mratibu wa kongamano
Cynthia Henjewelle
Akitaniana na wafanyakazi wa Uchumi Supermarket
No comments:
Post a Comment