Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa
jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Katibu wake Bw. Idd Swala huku
Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akisikiliza kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo Bw.ndugu Majid Mwanga.
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa jimbo la Chalinze akizungumza jambo na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga.
Mh. Ridhiwania Kikwete ametanganza rasmi jana katika mkutano huo
nia yake ya kutetea jimbo la Chalinze ambapo leo mchana anatarajiwa
kuchukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Bagamoyo tayari kwa kuanza
mchakato wa kuwania tena ubunge wa jimbo la Chalinze ili kuendeleza yale
aliyokwishayaanza kutekeleza katika kipidi cha mwaka mmoja alipokuwa
madarakani.
Diwani wa Kata ya Bwilingu Ahmed Nasser akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ndugu Majid Mwanga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jana.
Mh. Ridhiwani Kikwete mbunge wa
jimbo la Chalinze akizungumza na wananchi mjini Chalinze wakati
alipotangaza nia yake ya kutetea tena ubunge wa jimbo hilo.
Wananchi wa Chalinze
wakimsikiliza Ridhiwania Kikwete mbunge wa jimbo hilo hayupo pichani
wakati alipokuwa akitangaza nia yake ya kutetea tena kiti cha ubunge wa
jimbo la Chalinze.
No comments:
Post a Comment