Baadhi
ya watazamaji waliojitokeza katika kushuhudia mtanange wa washiriki
wanaaga mashindano katika wiki hii na kushuhudia wanaoingia katika jua
la utosi
Walimu
wa Washiriki wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke kutoka Kushoto Ni
Mwl Issa na Dkt Mona Mwakalinga wakifuatilia kazi ya wanafunzi wao
katika kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke
Majaji
wa Shindano la TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia show ya washiriki
wa TMT waliobahatika kuendelea na shindano hilo mara baada ya washiriki
wengine kuaga mashindano hayo kutokana na kura kutotosha.
Mahosti
wa Kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke wakifurahia kazi yao wakati wa
kipindi cha TMT kinachorushwa kila jumapili saa tatu na nusu usiku
kupitia kituo cha ITV
Baadhi ya washiriki wa TMT 2015 #mpakakieleweke wakiwa mbele ya majaji tayari kwa kutaja waliongia hatua ya jua la utosi.
Na Mwandishi Wetu
Shindano
la TMT 2015 #mpakakieleweke limeingia hatua nyingine tena mara baada ya
washiriki wengine kuaga shindano hilo . Katika hatua hiyo ya mchujo
hali imezidi kuwa ngumu kwa washiriki kutokana na shindano kuwa gumu
kwao kila wiki. Mpaka sasa jumla ya washiriki wanne wameshaaga shindano
hilo huku mchuano ukiwa mkali kwa washiriki waliobakia.
Ili
kuweza kumbakiza mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kumpigia
kura kadri uwezavyo ili kumnusuru na kuaga shindano ambalo limejizolea
umaarufu mkubwa ndani na nje ya Nchi ya Tanzania kutokana na ubora wake
na uwajibikaji na ubunifu wa shindano hilo
Jinsi
ya kumpigia kura mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika
ujumbe mfupi wa Maneno TMT ikifuatiwa na namba ya mshiriki halafu tuma
kwenda namba 0784 36 77 38.
Kufahamu
ni nani na nani wameaga shindano hili kwa wiki hii basi usikose
kufuatilia kipindi cha TMT 2015 #mpakakieleweke kupitia kituo cha
runinga cha ITV kila siku ya Jumapili saa tatu na nusu usiku.
Shindano
la TMT limepigwa Tafu na I-View Studio, Precision Air, Global
Publishers, Paisha, Cam Gas, Radio One na ITV pamoja na Pepsi.
No comments:
Post a Comment