Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi
kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa
‘Frank’ alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi
aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo
Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi
kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la
sanaa ‘Frank’ alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi
wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo.
Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo
Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
Msanii
maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa ‘Frank’
akizungumza na waandishi wa habari alipotambulishwa mara baada ya
kujiunga na chama hicho.
MSANII maarufu wa filamu nchini,
Mohamed Mwikongi jina la sanaa ‘Frank’ amejiunga na chama kipya cha
siasa cha ACT Wazalendo. Frank amejiunga na chama hicho leo jijini Dar
es Salaam akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika hafla hiyo ya utambulisho
kiongozi mwingine ambaye ni Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa
NCCR Mageuzi, Deo Meck pia amejiunga na chama cha ACT Wazalendo na
kukabidhiwa kadi za chama hicho.
Akiwakabidhi kadi za
ACT-Wazalendo, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa leo
Makao Makuu ya ACT alisema wamewapokea wanachama hao wapya kwa mikono
miwili na wapo tayari kushirikiana nao ndani ya chama hicho. Alisema
kuna idadi kubwa ya vigogo kutoka vyama vingine ambao tayari wameomba
kujiunga na chama chao na taratibu zinafanywa kutambulishwa.
Akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali zikiweno za Udiwani, Ubunge na Urais.
Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji
huo wa fomu kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na
hadi sasa kuna baadhi ya majimbo na kata zina watia azma kuanzia wanne
mpaka tisa jambo ambalo alidai ni faraja kwa ACT Wazalendo.
“Kati ya majimbo 265 yakiwamo
majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na waweka azma zaidi ya mmoja
katika majimbo 226 kwa nchi nzima na tunaamini mpaka kufikia mwisho wa
uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265 yatakuwa yanawatia azma
mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu,”
aliongeza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.
No comments:
Post a Comment