Kituo cha sheria na
haki za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na mashirika mengine yanayotetea haki
za raia leo wamefungua kesi ya kikatiba katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi
ya sheria ya kura ya maoni namba 11 ya
mwaka 2013 sheria ambayo wamedai inavunja haki za msingi za Raia wa Tanzania ambao
wapo katika kuamua hatma ya Taifa lao kupitia mchakato wa katiba mpya.
Akizungumza mahakamani
hapo na mtandao huu mara baada ya kufungua kesi hii mwanasheria kutoka kituo
cha sheria na haki za Binadamu LHRC HAROLD SUNGUSIA amesema kuwa kituo hicho kwa kushirikiana na mashirika mengine
walipokea mteja ambaye alijimbulisha kama mwananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
ndugu RASHID SALUM ambaye alitaka
kufunguliwa kwa shauri la kikatiba katika mahakama kuu ya Tanzania kuiomba
mahakama iweze kuamua juu ya ubatili wa baadhi ya vifungu vya sheria ya kura ya
maoni namba 11 ya mwaka 2013 ambazo amesema zinakinzana na haki za msingi za
raia katika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kwa mujibu wa
mwanasheria huyo vifungu vinavyolalamikiwa ni pamoja na kifungu cha 34 (2),(b)
ambacho kinatamka juu ya uhesabuji wa matokeo ya kura ya maoni kwa kujumuisha
kura za wananchi wasio raia wa Zanzibar kuweza kupiga na kuhesabiwa kura zao
kama wakazi wa Zanzibar ambapo amesema kifungu hicho kina lengo la kuwabagua
watanzania ambao ni wakazi wa Zanzibar na kuwanyima haki ya kuamua kwa uhuru
juu ya maswala yanayohusu muskabali wa taifa lao kwa kigezo cha uchache wao
dhidi ya wingi wa raia wa Tanzania bara kinyume na ibara ya 13(2) inayokataza
bunge kutunga sheria zenye ubaguzi dhidi ya raia na ibara ya 21(2) ya katiba ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 inayompa haki mwananchi kuamua juu ya
maswala ya taifa lake.
RASHID SALUM ambaye ni mwananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania aliyefungua shauri hilo leo akizungumza na wanahabari nje ya mahakama kuu Tanzania |
Akizungumza na mtandao
huu nje ya mahakama kuu jijini Dar es salaam mwananchi aliyewasilisha
malalamiko yake katika shirika hilo ndugu RASHID SALUM amesema kuwa ameamua
kufungua kesi hiyo ya kikatiba baada ya kugundua sheria hiyo ina madhara
makubwa katika mchakato wa katiba mpya kutokana na kuwa sheria hiyo inampa
mamlaka mwananchi wa Tanzania bara kumuwakilisha mkazi wa Zanzibar hata katika
kufanya maamuzi juu ya mambo yanayohusu taifa lao.
Amesema kuwa kifungu cha 37 cha sheria ya kura ya maoni kinatoa mwanya mkubwa wa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kusimamia zoezi nzima la kura ya maoni kutumia vibaya madaraka hayo katika kuwezesha mazingira maalum ya upigaji kura ya maoni kwa makundi maalum kinyume na ibara ya 29(5) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
No comments:
Post a Comment