Mjumbe wa kamayti ongozi ya TACCEO kutoka YOC PWANI bwana ISRAEL ILUNDE akizungumza na wanahabari katika mkutano huo kuhusu tathmini waliyoifanya katika zoezi hil. |
Wanahabari wakichukua Taarifa hiyo |
Wakati zoezi la
uandikishwaji wa daftari la kusumu la mpiga kura kwa mfumo mpya wa BVR likitarajiwa
kuingia Jijini Dar es salaam siku ya kesho baada ya kumaliza mikoani,tume ya
taifa ya uchaguzi imetakiwa kuhakikisha kuwa kasoro zilizojitokeza katika zoezi
hilo mikoani hazijirudii jijini Dar es salaam huku wakitakiwa kuhakikisha
wanawarudia wale ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha ili waweze kupata
haki hiyo.
Kauli hiyo imetolewa
leo Jijini Dar es salaam na mtandao wa Asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi
nchini Tanzania (TACCEO) unaoratibiwa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) wakati wakitoa tathmini yao kuhusu
mwenendo wa zoezi hilo lililokuwa linafanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
Mwenyekiti wa mtandao
huo Ms MARTINA KABISAMA amesema kuwa kumekuwa na
kasoro mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza wakati zoezi hilo likiendelea
katika mikoa mbalimbali jambo ambalo amesema limeathiri kwa kiasi kikubwa zoezi hilo kwa
baadhi ya mikoa hivyo kuitaka tume kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha
kuwa kasoro hizo hazijirudi.
Moja kati ya mapungufu
aliyoyataja ni pamoja na kukosekana kwa elimu ya mpiga kura kwa wananchi
mbalimbali ambapo amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa hawaelewi lengo kuu la
kujiandikisha huku wengine wakiamini kuwa kama wanamiliki kadi za zamani za kupigia
kura hawana haja ya kujiandikisha jambo ambalo limefanya wananchi wengi kuacha
kujiandikisha kwa kukosa elimu madhubuti juu ya hilo.
Katika dhana hiyo ya
kukosekana elimu ya mpiga kura Mwenyekiti huyo amesema kuwa kuna baadhi ya
maeneo wanakijiji wameshindwa kujitokeza katika zoezi hilo wakilifananisha na
zoezi hilo na maswala ya kichawi pamoja na FREMASON.
Ametolea mfano maeneo
ya mafia ambapo wananchi waligomea zoezi hilo wakilihusisha na imani za
Fremason,maeneo ya rufiji pale ambapo alama za vidole ziliposhindwa kutambuliwa
na mashine za BVR baadhi ya watu walisambaza uzushi kwamba watu hao ni
wachawi,huku kubwa zaidi ikiwa ni huko meru ambapo wananchi waligomea
kujiandikisha wakiamini kuwa mashine hizo zinanyonya damu.
Kasoro nyingine
zilizotajwa ni pamoja na vituo vya kujiandikisha kuwekwa katika nyumba za ibada,hospitali na
maeneo ya wazi,waandikishaji kutokuwa na elimu ya matumizi ya mashine za
BVR,Baadhi ya vituo kutokuwa na mazingira rafiki kwa walemavu,wazee na
wajawazito,kuharibika mara kwa mara kwa mashine za BVR kutokana na kufanya kazi
kwa muda mrefu,ukosefu wa utaratibu maalum wa uandikishwaji,pamoja na
kubadilika mara kwa mara kwa ratiba ya uandikishwaji jambo ambalo amesema pia
limewafanya watu wengi kushindwa kujiandikisha.
Aidha kasoro nyingine
ambazo zimetajwa kama kikwazo katika mchakato huo ni kukosekana kwa vifaa
muhimu kwenye mashine za BVR,pamoja na tume kushindwa kabisa kuonyesha jitihada
za dhati kwa wanafunzi wa vyuo,wagonjwa,na mahabusu walio magerezani ambao hadi
sasa hawajaandikishwa na hakuna dalili za wao kupata haki hiyo ya msingi.
Ms KABISAMA amesema
kuwa kutokana na kasoro hizo nyingi zilizojitokeza katika mchakato huo kuna
idadi kubwa ya watanzania ilishindwa kujiandikisha hivyo kama tume hiyo ina
dhamira ya dhati ya kuhakikisha watanzania wanapata haki hiyo ni lazima
wahakikisha kuwa wanawarudia wale ambao walishindwa kujiandikisha ili wapate
haki hiyo.
Jiji la Dar es salaam
linaingia katika siku yake ya kwanza kesho ya uandikishwaji wa dafrati la
kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR hii ikiwa ni baada ya zoezi hilo kupita
katika mikoa mingine ya Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment