MBUNGE wa Viti Maalum, Mariam Mfaki (CCM), amefariki dunia leo mchana katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alipokuwa amelazwa.
Marehemu amekuwa mbunge kwa vipindi vitatu, 2010 - 2015, 2005 - 2010 na 2000 - 2005.
Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mohammed Mfaki amesema mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2012.
Mfaki alisema mama yake atazikwa keshi shambani kwake katika eneo la Miyuji baada ya sala ya Alasiri itakayofanyika katika msikiti wa Nunge, mjini Dodoma.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Amen
No comments:
Post a Comment