MEYA wa jiji
la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo kupitia tiketi
ya chama cha Mapinduzi (CCM) akiahidi kuwafikisha wananchi wajimbo hilo katika
uchumi wa kati.
Amesema hayo
jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanafunzi waliopo katika vyuo
vya elimu ya juu ambao vyuo vyao viko katika jimbo hilo pamoja
na baadhi ya wananchi.
“Nimekuwa
kiongozi katika maeneo
mbalimbali…viongozi waliotangulia wamefanya kazi kubwa katika kuweka misingi imara
na sera mbalimbali za kuwaondoa wananchi
kutoka eneo moja hadi lingine,” alisema
Dk. Masaburi.
Alisema
pindi akichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo anawahakikshia wakazi wa Ubungo
kuwa atafanya kazi za kibunge kikamilifu akiwataka kufahamu kuwa yeye ni kitu chenye thamani na hatowaaangusha
katika majumuku yake.
Alisisitiza wananchi
ni lazima kuchagua kiongozi ambaye anaweza kuwaondoa kutoka hatua waliyomo na
kuwafiisha nyingine ambayo itaendelea kuwasaidia kuwaletea maendeleo kiuchumi na hata kijamii pia .
No comments:
Post a Comment