Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,
Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za
maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Ambapo amefafanua kuwa shughuli
zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi na
kumalizika saa sita mchana, pia wananchi watakaohudhuria kumbukumbu hiyo
watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea uwanjani
hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote muhimu ya
uwanja.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya
Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
……………………………………………………………..
Na.Aron Msigwa – MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk.Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika
Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayofanyika Julai 25,
2015 Katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya
kukamilika kwa maandalizi ya maadhimisho hayo leo jijini Dar es
salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema
maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam kuwakumbuka na
kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga kupigania uhuru na ukombozi wa
Taifa la Tanzania,kulinda na kudumisha amani na utulivu wa nchi.
Amesema Maadhimisho hayo
yatapambwa na Gwaride la Kumbukumbu litakaloandaliwa na vikosi vya Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi ,Magereza na Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT).
Aidha, amesema kutakuwa na
Mizinga salama itakayopigwa, uwekaji wa silaha za asili na maua kwenye
mnara wa kumbukumbu, Kutakuwa na sala na Dua kutoka kwa viongozi wa
Madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini.
Bw. Sadiki amefafanua kuwa
shughuli zote katika viwanja vya Mnazi Mmoja zitaanza saa mbili Asubuhi
na kumalizika saa sita mchana ambapo wananchi watakaohudhuria kumbukumbu
hiyo watapata fursa ya kushuhudia matukio yatakayokuwa yananendelea
uwanjani hapo kupitia Luninga kubwa zitakazokuwepo katika maeneo yote
muhimu ya uwanja.
Ameongeza kuwa siku hiyo baadhi
ya barabara katika jiji la Dar es Salaam zikiwemo Lumumba ,Uhuru na
Bibi Titi zitafungwa kwa muda ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wa
barabara hizo watakaohudhuria maadhimisho hayo .
Katika hatua nyingine Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam ametoa ufafanuzi kuhusu changamoto zinazoendelea
kujitokeza za kusuasua kwa zoezi uandikishaji wa wananchi katika daftari
la kudumu la wapiga kura katika mfumo wa BVR jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Manispaa za jiji la
Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia matatizo mbalimbali
yaliyojitokeza katika siku ya kwanza na ya pili katika baadhi ya vituo
hususani baadhi ya mashine za BVR kushindwa kufanya kazi vizuri.
Akizungumzia baadhi ya
malalamiko yanayotolewa na wananchi hasa tatizo la uchelewaji wa
waandikishaji kufika katika vituo walivyopangiwa kwa wakati amesema kuwa
Serikali ianaendelea kuchukua hatua ili kukomesha tabia hiyo.
Amewaagiza Wakurugenzi wa
Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwachukulia hatua watumishi hao
wazembe kwa kuwafuta kazi ili kuepusha madhara na vurugu zinazoweza
kuepukika na uongeza kuwa kazi ya uandikishaji wananchi inatakiwa kuanza
saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni kila siku kwa tarehe zilizopangwa.
Kuhusu taarifa za uwepo wa
baadhi ya watendaji kuwaingiza waandikishaji wasiohusika kusimamia zoezi
hilo Mkuu wa Mkoa huo amewataka watendaji hao kuacha mara moja tabia
hiyo ili kuepuka kuvuruga zoezi hilo na kwamba hatua kali za kisheria
zitachuliwa dhidi yao.
Pia amevitaka Vyama vya siasa
kuacha kutumia mwanya huo kuweka bendera au kuvaa mavazi yanayoashiria
kampeni za siasa ili kuepusha vurugu
No comments:
Post a Comment