Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina
akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar
hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama
hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na kujiunga na UKAWA
kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya uanachama hivi
karibu,jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi
mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na
Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo
Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya
Urais kupitia chama hicho,Mhe.Lowassa amekihama chama chake cha CCM na
kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA na kukabidhiwa kadi ya
uanachama hivi karibu,jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu WA Zamani Edward Lowassa akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa
CHADEMA, Mh. Tundu Lissu wakati alipofika kwenye Makao Makuu ya Chama
hicho tayari kwa kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia
Chama hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
Naibu
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Salum Mwalim akizungumza jambo katika kikao
kifupi ndani ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, kwenye makao Makuu ya
Chama hicho, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akisisitiza jambo kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA - Zanzibar, Salum Mwalim.
Mwanasheria
Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akitoa ufafanuzi wa kisheria wakati wa
hafla fupi ya kumkabidhi fomu ya kuwania Urais wa Tanzania, Waziri Mkuu
Mstaafu, Mh. Edward Lowassa.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akifafanua jambo.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akimkabidhi Fomu ya kuwania Urais wa Tanzania kupia Chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akionyesha Fomu ya Kuwania Urais wa
Tanzania kupitia CHADEMA, leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho,
Kinondoni Jijini Dar.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fedha za kuchukulia Fomu ya
Kuwania Urais kutoka kwa WamaCHADEMA waliojitolea kumlipia.
People'ssssss..........
Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akizungumza machache.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akionyesha Fomu kwa wanaCHADEMA
waliofurika kwa wingi kwenye Makao Makuu ya CHADEMA leo. Wengine pichani
toka kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe, Mama Regina Lowassa na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Zanzibar, Salum Mwalim.
CHANZO: MUHIDIN MICHUZI
No comments:
Post a Comment